Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 8:7 - Swahili Revised Union Version

7 Nikamwona akimkaribia kondoo dume, akamwonea hasira kali, akampiga kondoo dume, akazivunja pembe zake mbili; na huyo kondoo dume alikuwa hana nguvu kusimama mbele yake; bali akamwangusha chini, akamkanyagakanyaga; wala hapakuwapo awezaye kumwokoa kondoo dume katika mkono wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Nilimwona akimsogelea yule kondoo dume. Alikuwa amemkasirikia sana yule kondoo dume, hivyo akamshambulia kwa nguvu na kuzivunja zile pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuweza kustahimili. Alibwagwa chini na kukanyagwakanyagwa, wala hapakuwa na yeyote wa kumwokoa katika nguvu zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Nilimwona akimsogelea yule kondoo dume. Alikuwa amemkasirikia sana yule kondoo dume, hivyo akamshambulia kwa nguvu na kuzivunja zile pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuweza kustahimili. Alibwagwa chini na kukanyagwakanyagwa, wala hapakuwa na yeyote wa kumwokoa katika nguvu zake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Nilimwona akimsogelea yule kondoo dume. Alikuwa amemkasirikia sana yule kondoo dume, hivyo akamshambulia kwa nguvu na kuzivunja zile pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuweza kustahimili. Alibwagwa chini na kukanyagwakanyagwa, wala hapakuwa na yeyote wa kumwokoa katika nguvu zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Nikamwona akimshambulia yule kondoo dume kwa hasira nyingi, akampiga yule kondoo dume na kuvunja pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuwa na nguvu za kumzuia yule beberu; huyo beberu akamwangusha yule kondoo dume chini na kumkanyaga, wala hakuna aliyeweza kumwokoa yule kondoo dume kutoka nguvu za huyo beberu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Nikamwona akimshambulia yule kondoo dume kwa hasira nyingi, akimpiga yule kondoo dume na kuvunja pembe zake mbili. Yule kondoo dume hakuwa na nguvu za kumzuia yule beberu, hivyo akamwangusha yule kondoo dume chini na kumkanyaga, wala hakuna aliyeweza kumwokoa yule kondoo dume kutoka nguvu za huyo beberu.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

7 Nikamwona, alivyomfikia yule dume la kondoo, akamrukia kwa ukali mwenye uchungu, akampiga yule dume la kondoo, akazivunja pembe zake mbili, naye dume la kondoo hakuwa na nguvu ya kusimama mbele yake, kwa hiyo akambwaga chini, akamkanyagakanyaga, tena hakuwako aliyemwokoa yule dume la kondoo mkononi mwake.

Tazama sura Nakili




Danieli 8:7
8 Marejeleo ya Msalaba  

Na mfalme wa kusini ataingiliwa na ghadhabu, naye atatoka na kupigana naye, yaani, na mfalme wa kaskazini; naye atapanga jeshi kubwa; na jeshi hilo litawekwa mikononi mwake.


Na kwa habari za wale wanyama wengine, walinyang'anywa mamlaka yao; lakini maisha yao yalidumishwa kwa wakati na majira.


Baadaye nikaona katika njozi ya usiku, na tazama, mnyama wa nne, mwenye kutisha, mwenye nguvu, mwenye uwezo mwingi, naye alikuwa na meno ya chuma, makubwa sana; alikula na kuvunja vipande vipande, na kuyakanyaga mabaki kwa miguu yake; na umbo lake lilikuwa mbali kabisa na wale wa kwanza, naye alikuwa na pembe kumi.


Nayo ikakua, kiasi cha kulifikia jeshi la mbinguni; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na ya nyota, ikazikanyaga.


Naye akamwendea huyo kondoo dume mwenye pembe mbili, niliyemwona akisimama karibu na mto, akamshambulia kwa ghadhabu za nguvu zake.


Na yule beberu akajitukuza sana; na alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ilivunjika; na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni.


Nao wataangukiana wenyewe kwa wenyewe, kama mbele ya upanga, hapo ambapo hapana afukuzaye; wala hamtakuwa na nguvu za kusimama mbele ya adui zenu.


Kisha hapo hao watu wa Ai walipotazama nyuma yao, wakaona, na tazama, moshi wa huo mji ulikuwa unapaa juu kwenda mawinguni, nao hawakuwa na nguvu za kukimbia huku wala huku; na wale watu waliokuwa wamekimbia kwenda nyikani wakageuka na kuwarudia hao waliokuwa wakiwafuatia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo