Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 8:5 - Swahili Revised Union Version

5 Nami nilipokuwa nikifikiri, tazama, beberu akatoka upande wa magharibi, juu ya uso wa dunia nzima, bila kuigusa nchi; na beberu yule alikuwa na pembe mashuhuri kati ya macho yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 “Nilipokuwa ninawaza juu ya jambo hili, niliona beberu mmoja kutoka upande wa magharibi akija kasi bila kugusa ardhi. Kati ya macho yake alikuwa na pembe moja kubwa sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 “Nilipokuwa ninawaza juu ya jambo hili, niliona beberu mmoja kutoka upande wa magharibi akija kasi bila kugusa ardhi. Kati ya macho yake alikuwa na pembe moja kubwa sana.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 “Nilipokuwa ninawaza juu ya jambo hili, niliona beberu mmoja kutoka upande wa magharibi akija kasi bila kugusa ardhi. Kati ya macho yake alikuwa na pembe moja kubwa sana.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Nilipokuwa ninatafakari hili, ghafula beberu mwenye pembe moja kubwa katikati ya macho yake alikuja kutoka magharibi, akiruka kasi juu ya dunia yote bila kugusa ardhi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Nilipokuwa ninatafakari hili, ghafula beberu mwenye pembe moja kubwa sana katikati ya macho yake alikuja kutoka magharibi, akiruka kasi juu ya dunia yote bila kugusa ardhi.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

5 Nilipokuwa sijamtambua vema, mara nikaona dume la mbuzi aliyetoka machweoni kwa jua, akapita juu ya nchi yote nzima pasipo kugusa mchanga wa chini kwa miguu; huyo dume la mbuzi alikuwa na pembe kubwa mno katikati ya macho yake.

Tazama sura Nakili




Danieli 8:5
7 Marejeleo ya Msalaba  

Na mfalme hodari atasimama, atakayetawala kwa uwezo mkuu, na kutenda apendavyo.


Na sanamu hii kichwa chake kilikuwa ni cha dhahabu safi; kifua chake na mikono yake ni ya fedha; tumbo lake na viuno vyake ni vya shaba;


Na baada yako utainuka ufalme mwingine mdogo kuliko wewe; na ufalme mwingine wa tatu wa shaba, utakaoitawala dunia yote.


Kisha nikatazama, na kumbe! Mnyama mwingine, kama chui, naye juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege; mnyama huyo alikuwa na vichwa vinne; akapewa mamlaka.


Na yule beberu, mwenye manyoya mengi, ni mfalme wa Ugiriki; na ile pembe kubwa iliyo kati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.


Naye akamwendea huyo kondoo dume mwenye pembe mbili, niliyemwona akisimama karibu na mto, akamshambulia kwa ghadhabu za nguvu zake.


Na yule beberu akajitukuza sana; na alipokuwa na nguvu, pembe ile kubwa ilivunjika; na badala yake zikazuka pembe nne mashuhuri zilizoelekea pepo nne za mbinguni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo