Danieli 6:22 - Swahili Revised Union Version22 Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye amevifunga vinywa vya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nilionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema22 Mungu wangu alileta malaika wake kuvifumba vinywa vya simba hawa, nao hawakunidhuru. Alifanya hivyo kwa sababu alijua mimi sina lawama yoyote kwake na wala sijafanya lolote baya mbele yako.” Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND22 Mungu wangu alileta malaika wake kuvifumba vinywa vya simba hawa, nao hawakunidhuru. Alifanya hivyo kwa sababu alijua mimi sina lawama yoyote kwake na wala sijafanya lolote baya mbele yako.” Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza22 Mungu wangu alileta malaika wake kuvifumba vinywa vya simba hawa, nao hawakunidhuru. Alifanya hivyo kwa sababu alijua mimi sina lawama yoyote kwake na wala sijafanya lolote baya mbele yako.” Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu22 Mungu wangu alimtuma malaika wake, naye akafunga vinywa vya hawa simba. Hawajanidhuru, kwa sababu nilionekana sina hatia mbele zake. Wala kamwe sijafanya jambo lolote baya mbele yako, ee mfalme.” Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu22 Mungu wangu alimtuma malaika wake, naye akafunga vinywa vya hawa simba. Hawajanidhuru, kwa sababu nilionekana sina hatia mbele zake. Wala kamwe sijafanya jambo lolote baya mbele yako, ee mfalme.” Tazama suraSwahili Roehl Bible 193722 Mungu ametuma malaika wake, akavifumba vinywa vya simba, hawakuniumiza, kwa kuwa mbele yake nimeonekana kuwa mtu asiyekosa; hata mbele yako, mfalme, hakuna kiovu, nilichokifanya. Tazama sura |
Mawaziri wote wa ufalme, na wasimamizi, na viongozi, na washauri, na watawala wamefanya shauri pamoja ili kuweka amri ya kifalme; na kupiga marufuku, ya kwamba mtu yeyote atakayeomba dua kwa Mungu awaye yote, au kwa mtu awaye yote, katika muda wa siku thelathini, ila kwako, Ee mfalme atatupwa katika tundu la simba.