Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 12:13 - Swahili Revised Union Version

13 Lakini nenda zako hata utakapokuwa mwisho ule; maana wewe utastarehe, nawe utaamka katika kura yako mwisho wa siku hizo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 “ ‘Lakini wewe, ee Danieli, jiendee, ukapumzike kaburini, na wakati huo utakapotimia, utafufuka na kupata tuzo lako.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 “ ‘Lakini wewe, ee Danieli, jiendee, ukapumzike kaburini, na wakati huo utakapotimia, utafufuka na kupata tuzo lako.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 “‘Lakini wewe, ee Danieli, jiendee, ukapumzike kaburini, na wakati huo utakapotimia, utafufuka na kupata tuzo lako.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 “Lakini wewe, nenda zako hadi mwisho. Utapumzika, nawe mwisho wa hizo siku utafufuka ili kuupokea urithi uliowekewa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 “Lakini wewe, enenda zako mpaka mwisho. Utapumzika, nawe ndipo mwisho wa hizo siku utafufuka ili kuupokea urithi uliowekewa.”

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

13 Basi, wewe jiendee, uufikie mwisho! Utatulia, upate kuliinukia fungu lako, siku za mwisho zitakapotimia.

Tazama sura Nakili




Danieli 12:13
16 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.


BWANA ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unayaamua maisha yangu.


Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nayo nafsi yangu inashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.


Akasema, Uso wangu utakwenda pamoja nawe, nami nitakupa raha.


Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.


Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka.


BWANA wa majeshi asema hivi, Ikiwa utaenda katika njia zangu, na kushika maagizo yangu, basi utaihukumu nyumba yangu, na kuzilinda nyua zangu, nami nitakupa haki ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.


Yesu akawaambia, Amin, nawaambia ya kwamba ninyi mlionifuata mimi, katika ulimwengu mpya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti kumi na viwili, mkiwahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.


Basi, kesheni ninyi kila wakati, mkiomba, ili mpate kuokoka katika haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.


Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.


na kuwalipa ninyi mteswao raha pamoja na sisi; wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake,


Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo