Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 10:3 - Swahili Revised Union Version

3 Sikula chakula kitamu, wala nyama wala divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Sikula chakula cha fahari, sikugusa nyama wala divai, na sikujipaka mafuta kwa muda wa majuma hayo yote matatu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Sikula chakula cha fahari, sikugusa nyama wala divai, na sikujipaka mafuta kwa muda wa majuma hayo yote matatu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Sikula chakula cha fahari, sikugusa nyama wala divai, na sikujipaka mafuta kwa muda wa majuma hayo yote matatu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Sikula chakula kizuri; nyama wala divai havikugusa midomo yangu; nami sikujipaka mafuta kamwe hadi majuma matatu yalipotimia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Sikula chakula kizuri; nyama wala divai havikugusa midomo yangu; nami sikujipaka mafuta kamwe mpaka majuma matatu yalipotimia.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

3 Sikula chakula kilichopendeza, wala nyama, wala mvinyo haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta, mpaka siku za majuma matatua ziishe.

Tazama sura Nakili




Danieli 10:3
11 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Mefiboshethi, mwana wa Sauli, akashuka ili amlaki mfalme; alikuwa hakukata kucha za miguu yake wala kukata ndevu zake, wala kufua nguo zake, tangu siku alipoondoka mfalme, hadi siku hiyo aliporudi kwake kwa amani.


Hata roho yake huchukia chakula, Na nafsi yake huchukia nyama nzuri.


Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.


na miungu yao, pamoja na sanamu zao, na vyombo vyao vizuri vya fedha na dhahabu atavichukua mpaka Misri; kisha atajizuia miaka kadhaa asimwendee mfalme wa kaskazini.


Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.


Basi, kwa kuwa mnamkanyaga maskini, na kumtoza ngano; ninyi mmejenga nyumba za mawe yaliyochongwa, lakini hamtakaa ndani yake; ninyi mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu, lakini hamtakunywa divai yake.


Chukueni nyara za fedha; Chukueni nyara za dhahabu; Kwa maana ni akiba isiyoisha, Fahari ya vyombo vipendezavyo.


Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;


Hukunipaka kichwa changu mafuta; bali huyu amenipaka miguu yangu marhamu.


bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiria wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo