Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 1:8 - Swahili Revised Union Version

8 Lakini Danieli aliazimu moyoni mwake ya kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme, wala kwa divai aliyokunywa; basi akamwomba yule mkuu wa matowashi ampe ruhusa asijitie unajisi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Lakini Danieli aliamua kutojitia unajisi kwa kula chakula bora cha mfalme na kunywa divai yake. Kwa hiyo, alimwomba towashi mkuu amruhusu asile vitu hivyo na kujitia unajisi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Lakini Danieli aliamua kutojitia unajisi kwa kula chakula bora cha mfalme na kunywa divai yake. Kwa hiyo, alimwomba towashi mkuu amruhusu asile vitu hivyo na kujitia unajisi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Lakini Danieli aliamua kutojitia unajisi kwa kula chakula bora cha mfalme na kunywa divai yake. Kwa hiyo, alimwomba towashi mkuu amruhusu asile vitu hivyo na kujitia unajisi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Lakini Danieli alikusudia kuwa hatajinajisi kwa chakula cha mfalme na divai, naye akamwomba mkuu wa maafisa ruhusa ili asijinajisi kwa njia hii.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Lakini Danieli alikusudia kuwa hatajitia unajisi kwa chakula cha mfalme na divai, naye akamwomba mkuu wa maafisa ruhusa ili asijinajisi kwa njia hii.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

8 Lakini Danieli alisema moyoni mwake: Sitajipatia uchafu nikila vilaji vya urembo vya mfalme au nikinywa mvinyo zake; akamwomba mkuu wa watumishi wa nyumbani ruhusa, asijipatie uchafu hivyo.

Tazama sura Nakili




Danieli 1:8
22 Marejeleo ya Msalaba  

Nami, tazama, nakusudia kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wangu, kama BWANA alivyomwambia Daudi baba yangu, akisema, Mwana wako, nitakayemweka katika kiti chake cha enzi mahali pako, ndiye atakayeijenga nyumba kwa jina langu.


Wakamwabudu Baal-Peori, Wakazila dhabihu zilizotolewa kwa wafu.


Nimeapa nami nikathibitisha, Kuzishika hukumu zako za haki.


Enyi watenda mabaya, ondokeni kwangu, Niyashike maagizo ya Mungu wangu.


Usiuelekeze moyo wangu kunako jambo baya, Nisiyazoelee matendo yasiyofaa, Pamoja na watu watendao maovu; Wala nisile vyakula vyao vya anasa.


Usivitamani vyakula vyake vya anasa; Kwa maana ni vyakula vya hila.


Huyo mfalme akawaagizia wapewe chakula kama cha mfalme, na divai aliyokunywa, akaagiza walishwe hivyo muda wa miaka mitatu; ili kwamba hatimaye wasimame mbele ya mfalme.


Wakanywa divai, wakaisifu miungu ya dhahabu, na ya fedha, na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe.


Naye, alipofika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa moyo wote.


bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu.


Lakini yeye aliyesimama kwa uthabiti wa moyo wake, hana sharti, lakini aweza kuyatawala mapenzi yake, tena amekusudia moyoni mwake kumlinda mwanamwali wake, atatenda vema.


Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.


Uliokula shahamu za sadaka zao, Na kunywa divai ya sadaka zao za kinywaji? Na waondoke na kuwasaidia ninyi; Na wawe hao himaya yenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo