Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Amosi 5:26 - Swahili Revised Union Version

26 Naam, mtamchukua Sikuthi, mfalme wenu, na Kiuni, sanamu zenu, nyota ya mungu wenu, mliojifanyia wenyewe.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Je, wakati huo mlibeba kama sasa vinyago vya mungu wenu Sakuthi mfalme wenu na vinyago vya Kaiwani mungu wenu wa nyota, vitu ambavyo mlijitengenezea wenyewe?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Je, wakati huo mlibeba kama sasa vinyago vya mungu wenu Sakuthi mfalme wenu na vinyago vya Kaiwani mungu wenu wa nyota, vitu ambavyo mlijitengenezea wenyewe?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Je, wakati huo mlibeba kama sasa vinyago vya mungu wenu Sakuthi mfalme wenu na vinyago vya Kaiwani mungu wenu wa nyota, vitu ambavyo mlijitengenezea wenyewe?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Mmeyainua madhabahu ya Sikuthi mungu wenu mtawala, na Kiuni mungu wenu wa nyota, ambao mliwatengeneza wenyewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Mmeyainua madhabahu ya mfalme wenu, Sikuthi mungu wenu mtawala, na Kiuni mungu wenu wa nyota, ambao mliwatengeneza wenyewe.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 Naam, mtamchukua Sikuthi, mfalme wenu, na Kiuni, sanamu zenu, nyota ya mungu wenu, mliojifanyia wenyewe.

Tazama sura Nakili

Amosi 5:26
7 Marejeleo ya Msalaba  

kwa sababu wameniacha mimi wakaabudu Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Kemoshi, mungu wa Wamoabi, na Milkomu, mungu wa wana wa Amoni wala hawakuenda katika njia zangu, kutenda mema machoni pangu, kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, kama Daudi baba yake.

kwa sababu walizikataa hukumu zangu, wala hawakuenda katika amri zangu, wakazitia unajisi sabato zangu, kwa maana mioyo yao iliandama vinyago vyao.

Usimtoe kafara mzawa wako yeyote kwa Moleki na ulinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA.

Kwa sababu hiyo nitawapeleka uhamishoni, mwende mbali kupita Dameski, asema BWANA, ambaye jina lake ni Mungu wa majeshi.

Nanyi mlichukua hema ya Moleki, Na nyota za mungu wenu Refani, Sanamu mlizozifanya ili kuziabudu; Nami nitawafahamisha mwende mbali kupita Babeli.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo