Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Wafalme 8:10 - Swahili Revised Union Version

10 Elisha akamwambia, Nenda, ukamwambie, Bila shaka utapona; lakini BWANA amenionesha ya kwamba bila shaka atakufa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Basi Elisha akamjibu, “Atapona; lakini Mwenyezi-Mungu amenionesha kwamba atakufa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Basi Elisha akamjibu, “Atapona; lakini Mwenyezi-Mungu amenionesha kwamba atakufa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Basi Elisha akamjibu, “Atapona; lakini Mwenyezi-Mungu amenionesha kwamba atakufa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Al-Yasa akajibu, “Nenda ukamwambie, ‘Hakika utapona’; lakini Mwenyezi Mungu amenifunulia kwamba kweli atakufa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Al-Yasa akajibu, “Nenda ukamwambie, ‘Hakika utapona’; lakini bwana amenifunulia kwamba kweli atakufa.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Elisha akamwambia, Nenda, ukamwambie, Bila shaka utapona; lakini BWANA amenionesha ya kwamba bila shaka atakufa.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 8:10
16 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo utakufa hakika.”


Farao akamwambia Yusufu, Kwa kuwa Mungu amekufahamisha hayo yote, hapana mwenye akili na hekima kama wewe.


Na alipokuja kwa mfalme, mfalme alimwambia, Je! Mikaya, tuende Ramoth-Gileadi kupiga vita, au tunyamaze? Akamwambia, Kwea, ufanikiwe; kwa kuwa BWANA atautia mkononi mwa mfalme.


Akamwambia, BWANA asema hivi, Kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, je! Ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa.


Basi sasa, BWANA asema hivi, Hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa. Eliya akaondoka.


Lakini kama ukikataa kutoka, hili ndilo neno ambalo BWANA amenionesha;


Ndipo nikawaambia watu wa uhamisho habari ya mambo yote aliyonionesha BWANA.


naye amekopesha watu ili apate faida, na kupokea ziada; je! Ataishi baada ya hayo? La, hataishi; amefanya machukizo hayo yote; hakika atakufa; damu yake itakuwa juu yake.


Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.


Haya ndiyo aliyonionesha Bwana MUNGU; tazama, aliumba nzige mwanzo wa kuchipuka kwake mimea wakati wa vuli; na tazama, ilikuwa mimea ya wakati wa vuli baada ya mavuno ya mfalme.


Haya ndiyo aliyonionesha Bwana MUNGU; tazama, Bwana MUNGU aliita ili kushindana kwa moto; nao ukaviteketeza vilindi vikuu, ukataka kuiteketeza nchi kavu.


Haya ndiyo aliyonionesha; na tazama, Bwana alisimama karibu na ukuta uliojengwa kwa timazi, mwenye timazi mkononi mwake.


Haya ndiyo aliyonionesha Bwana MUNGU; tazama, kikapu cha matunda ya wakati wa joto.


Kisha BWANA akanionesha wafua chuma wanne.


Kisha akanionesha mto wa maji ya uzima, wenye kung'aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-kondoo,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo