Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Wafalme 10:17 - Swahili Revised Union Version

17 Naye alipofika Samaria, aliwaua wote wa Ahabu waliokuwa wamebakia katika Samaria, hata akamwangamiza, sawasawa na neno la BWANA alilomwambia Eliya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Walipofika Samaria, Yehu aliua jamaa yote ya Ahabu bila kumwacha hata mmoja wao. Ikawa sawa kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Elia itakavyokuwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Walipofika Samaria, Yehu aliua jamaa yote ya Ahabu bila kumwacha hata mmoja wao. Ikawa sawa kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Elia itakavyokuwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Walipofika Samaria, Yehu aliua jamaa yote ya Ahabu bila kumwacha hata mmoja wao. Ikawa sawa kama Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Elia itakavyokuwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Yehu alipofika Samaria, akawaua wale wote waliokuwa wamesalia wa jamaa ya Ahabu, akawaangamiza, sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu alilosema kupitia Ilya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Yehu alipofika Samaria, akawaua wale wote waliokuwa wamesalia wa jamaa ya Ahabu, akawaangamiza, sawasawa na neno la bwana alilosema kupitia Ilya.

Tazama sura Nakili




2 Wafalme 10:17
8 Marejeleo ya Msalaba  

Angalia, nitaleta mabaya juu yako; nami nitakuangamiza kabisa, nitamkatia Ahabu kila mwanamume, aliyefungwa na aliyeachwa katika Israeli.


Basi akafa, sawasawa na neno la BWANA alilolinena Eliya. Na Yoramu alianza kutawala mahali pake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda; kwa kuwa yeye hakuwa na mwana.


Kwa maana nyumba yote ya Ahabu wataangamia; nami nitamkatilia mbali kila mwanamume wa nyumba ya Ahabu, yeye aliyefungwa, na yeye asiyefungwa, katika Israeli.


Ikawa, Yehu alipokuwa akiwafanyia hukumu nyumba ya Ahabu, aliwakuta wakuu wa Yuda, na wana wa nduguze Ahazia, wakimtumikia Ahazia, akawaua.


Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuri; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo