Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Samueli 9:3 - Swahili Revised Union Version

3 Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu yeyote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Mfalme akamwuliza, “Je, hakuna mtu yeyote aliyesalia katika jamaa ya Shauli? Kama yuko, ningependa kumtendea wema wa Mungu.” Siba akamjibu, “Yuko mwana wa Yonathani, lakini yeye amelemaa miguu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Mfalme akamwuliza, “Je, hakuna mtu yeyote aliyesalia katika jamaa ya Shauli? Kama yuko, ningependa kumtendea wema wa Mungu.” Siba akamjibu, “Yuko mwana wa Yonathani, lakini yeye amelemaa miguu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Mfalme akamwuliza, “Je, hakuna mtu yeyote aliyesalia katika jamaa ya Shauli? Kama yuko, ningependa kumtendea wema wa Mungu.” Siba akamjibu, “Yuko mwana wa Yonathani, lakini yeye amelemaa miguu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Mfalme akamuuliza, “Je, hakuna yeyote ambaye amebaki wa nyumba ya Sauli ninayeweza kumwonesha wema wa Mungu?” Siba akamjibu mfalme, “Bado yupo mwana wa Yonathani; yeye ni kiwete kwenye miguu yote.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Mfalme akauliza, “Je, hakuna yeyote ambaye amebaki wa nyumba ya Sauli ninayeweza kumwonyesha wema wa Mungu?” Siba akamjibu mfalme, “Bado yupo mwana wa Yonathani, yeye ni kiwete miguu yote.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu yeyote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu.

Tazama sura Nakili

2 Samueli 9:3
11 Marejeleo ya Msalaba  

Naye akajibu, Bwana wangu, Ee mfalme, mtumishi wangu alinidanganya; kwa kuwa mimi mtumishi wako nilisema, Nitajitandikia punda, nipate kumpanda, na kwenda pamoja na mfalme; kwa sababu mimi mtumishi wako ni kiwete.

Naye amenisingizia mimi mtumishi wako kwa bwana wangu mfalme; lakini bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu; utende basi yaliyo mema machoni pako.

Naye Yonathani, mwana wa Sauli alikuwa na mwana aliyekuwa na kilema cha miguu. Alikuwa na umri wa miaka mitano, habari za Sauli na Yonathani zilipofika Yezreeli, na yaya wake akamchukua akakimbia ikawa, alipokimbia kwa haraka, huyo mtoto akaanguka, akawa kilema. Na jina lake aliitwa Mefiboshethi.

Basi Mefiboshethi akakaa Yerusalemu; maana alikuwa akila chakula siku zote mezani pa mfalme; naye alikuwa na kilema cha miguu yote miwili.

Daudi akamwambia, Usiogope, maana bila shaka nitakutendea mema; kwa ajili ya Yonathani, baba yako, nami nitakurudishia mashamba yote ya Sauli, babu yako; nawe utakula chakula mezani pangu daima.

Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.

Tena, BWANA aliwafurahia baba zako, na kuwapenda, akawachagua wazao wao baada yao, naam, na ninyi zaidi ya mataifa yote kama hivi leo.

Na kwa sababu aliwapenda baba zenu, kwa sababu hiyo aliwachagua wazao wao baada yao, akakutoa katika Misri kwa kuwako pamoja nawe, kwa uweza wake mwingi,

Tufuate:

Matangazo

Matangazo