Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Samueli 21:16 - Swahili Revised Union Version

16 Naye Ishi-benobu, aliyekuwa mmoja wa Warefai, ambaye uzito wa mkuki wake ulikuwa shekeli mia tatu za shaba kwa uzani, naye amejifungia upanga mpya, alijaribu kumwua Daudi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Ishbi-benobu, mmojawapo wa wazawa wa majitu ambaye mkuki wake wa shaba ulikuwa na uzito wa karibu kilo tatu na nusu na aliyekuwa amejifunga upanga mpya alisema atamuua Daudi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Ishbi-benobu, mmojawapo wa wazawa wa majitu ambaye mkuki wake wa shaba ulikuwa na uzito wa karibu kilo tatu na nusu na aliyekuwa amejifunga upanga mpya alisema atamuua Daudi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Ishbi-benobu, mmojawapo wa wazawa wa majitu ambaye mkuki wake wa shaba ulikuwa na uzito wa karibu kilo tatu na nusu na aliyekuwa amejifunga upanga mpya alisema atamuua Daudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Naye Ishbi-Benobu, mmoja wa wazao wa Warefai, ambaye mkuki wake ulikuwa na uzito wa shekeli mia tatu za shaba, alikuwa amejifunga upanga mpya, naye akasema atamuua Daudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Naye Ishbi-Benobu, mmoja wa wazao wa Warefai, ambaye mkuki wake ulikuwa na uzito wa shekeli 300 za shaba, alikuwa amejifunga upanga mpya, naye alisema angemuua Daudi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Naye Ishi-benobu, aliyekuwa mmoja wa Warefai, ambaye uzito wa mkuki wake ulikuwa shekeli mia tatu za shaba kwa uzani, naye amejifungia upanga mpya, alijaribu kumwua Daudi.

Tazama sura Nakili




2 Samueli 21:16
20 Marejeleo ya Msalaba  

Na mwaka wa kumi na nne akaja Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye, wakawapiga Warefai katika Ashteroth-karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, na Waemi katika Shawe-kiryathaimu,


Nao Wanefili walikuwako duniani siku zile; tena, baada ya hayo, wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.


Ikawa baada ya hayo, kulikuwa na vita tena na Wafilisti huko Gobu; ndipo Sibekai, Mhushathi, alipomwua Safu, aliyekuwa mmoja wa Warefai.


Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambako kulikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole sita katika kila mkono, na vidole sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne; yeye naye alizaliwa kwa Mrefai.


Hao wanne walizaliwa kwake huyo Mrefai wa Gathi; wakaanguka kwa mkono wa Daudi, na kwa mikono ya watumishi wake.


Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kujitawanya bondeni mwa Warefai.


Wakapanda katika Negebu, wakafika Hebroni; na Ahimani, na Sheshai, na Talmai, wana wa Anaki, walikuwako huko. Nao Hebroni ulijengwa miaka saba kabla ya Soani wa Misri.


Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni wenye nguvu, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na hayo tuliwaona wana wa Anaki huko.


Twakwea kwenda wapi? Ndugu zetu wameiyeyusha mioyo yetu, wakituambia, Wale watu ni wengi, ni warefu kuliko sisi; miji nayo ni mikubwa, imejengewa kuta hata mbinguni; na zaidi ya hayo huko tumewaona Waanaki.


(Walioishi humo hapo kale ni Waemi, nao ni watu wakubwa, wengi, warefu, mfano wa Waanaki;


na hawa nao wadhaniwa kuwa Warefai kama Waanaki; lakini Wamoabi huwaita Waemi.


nao ni watu wengi, wakubwa, warefu, kama Waanaki; lakini BWANA aliwaangamiza mbele yao; wakawafuata wakakaa badala yao;


(Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho kingali kiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni dhiraa tisa, na upana wake dhiraa nane, kwa mfano wa mkono wa mtu).


watu wakubwa, warefu, wana wa Waanaki, uwajuao, uliokuwa ukisikia wakitajwa hivi, Ni nani awezaye kusimama mbele ya wana wa Anaki?


Hawakusalia Waanaki hata mmoja katika nchi ya wana wa Israeli; isipokuwa walisalia katika Gaza, na katika Gathi, na katika Ashdodi.


Huyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wazawa wa Anaki.


Na mpini wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji; na kichwa cha mkuki wake kilikuwa shekeli mia sita za chuma uzito wake; na mtu aliyemchukulia ngao yake akamtangulia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo