Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




2 Samueli 20:19 - Swahili Revised Union Version

19 Mimi ni mmoja wa hao wenye amani, walio waaminifu katika Israeli; wewe unataka kuuharibu mji ulio kama mama wa Israeli; mbona unataka kuumeza urithi wa BWANA?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Mimi ni mmojawapo wa wale wanaopenda amani na uaminifu katika Israeli. Sasa wewe unakusudia kuuharibu mji ambao ni kama mama katika Israeli. Kwa nini sasa unataka kuuangamiza mji ulio mali yake Mwenyezi-Mungu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Mimi ni mmojawapo wa wale wanaopenda amani na uaminifu katika Israeli. Sasa wewe unakusudia kuuharibu mji ambao ni kama mama katika Israeli. Kwa nini sasa unataka kuuangamiza mji ulio mali yake Mwenyezi-Mungu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Mimi ni mmojawapo wa wale wanaopenda amani na uaminifu katika Israeli. Sasa wewe unakusudia kuuharibu mji ambao ni kama mama katika Israeli. Kwa nini sasa unataka kuuangamiza mji ulio mali yake Mwenyezi-Mungu?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Sisi ni watu wa amani na waaminifu katika Israeli. Wewe unajaribu kuharibu mji ambao ni mama katika Israeli. Kwa nini unataka kumeza urithi wa Mwenyezi Mungu?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Sisi ni watu wa amani na waaminifu katika Israeli. Wewe unajaribu kuharibu mji ambao ni mama katika Israeli. Kwa nini unataka kumeza urithi wa bwana?”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

19 Mimi ni mmoja wa hao wenye amani, walio waaminifu katika Israeli; wewe unataka kuuharibu mji ulio kama mama wa Israeli; mbona unataka kuumeza urithi wa BWANA?

Tazama sura Nakili




2 Samueli 20:19
29 Marejeleo ya Msalaba  

Abrahamu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu?


Kwa kuwa mfalme atasikia, ili amwokoe mtumishi wake mkononi mwa yule mtu atakaye kuniharibu mimi na mwanangu pia katika urithi wa Mungu.


Basi sasa pelekeni habari upesi, kamwambieni Daudi ya kwamba, Usilale usiku huu karibu na vivuko vya jangwani; bali usikose kuvuka; asije akamezwa mfalme, na watu wote walio pamoja naye.


Kisha akanena, akisema, Watu hunena zamani za kale, wakisema, Wasikose kuuliza huko Abeli; ndivyo walivyoleta suluhu.


Yoabu akajibu, akasema, Isiwe, isiwe kwangu, niumeze wala kuuharibu.


basi Daudi akawaambia hao Wagibeoni, Niwatendee nini? Na kwa tendo gani nifanye upatanisho, mpate kuubariki urithi wa BWANA?


Kwa maana uliwatenga na watu wote wa dunia, wawe urithi wako, kama ulivyonena kwa mdomo wa Musa, mtumishi wako, hapo ulipowatoa baba zetu katika Misri, Ee Bwana MUNGU.


Ili niuone wema wa wateule wako. Nipate kuifurahia furaha ya taifa lako, Na kujisifu pamoja na watu wako.


Papo hapo wangalitumeza hai, Hasira yao ilipowaka juu yetu.


Heri taifa ambalo BWANA ni Mungu wao, Watu aliowachagua kuwa urithi wake.


Nyuma ya kondoo wanyonyeshao alimwondoa, Awachunge Yakobo watu wake, na Israeli urithi wake.


Nebukadneza, mfalme wa Babeli, amenila, ameniponda, amenifanya kuwa chombo kitupu; amenimeza kama joka, amelijaza tumbo lake vitu vyangu vya anasa; amenitupa


Nami nitafanya hukumu juu ya Beli katika Babeli, nami nitavitoa katika kinywa chake alivyovimeza; wala mataifa hawatamwendea tena; naam, ukuta wa Babeli utaanguka.


Juu yako adui zako wote Wamepanua vinywa vyao; Huzomea, husaga meno yao, Husema, Tumemmeza; Hakika siku hii ndiyo tuliyoitazamia; Tumeipata, tumeiona.


Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo, Wala hakuona huruma; Ameziangusha ngome za binti Yuda Katika ghadhabu yake; Amezibomoa hata nchi Ameunajisi ufalme na wakuu wake.


Bwana amekuwa mfano wa adui, Amemmeza Israeli; Ameyameza majumba yake yote, Ameziharibu ngome zake; Tena amemzidishia binti Yuda Matanga na maombolezo.


nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.


nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara.


Basi huu uharibikao utakapovaa kutoharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa katika ushindi.


Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twapumua kwa shida, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.


Utakaposongea karibu ya mji kwenda kupigana juu yake, ndipo utakapowapigia ukelele wa amani.


Maana, sehemu ya BWANA ni watu wake, Yakobo ni kura ya urithi wake.


kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.


Watawala walikoma katika Israeli, walikoma, Hadi mimi Debora nilipoinuka, Nilipoinuka mimi, mama katika Israeli.


Ndipo Samweli akatwaa kichupa cha mafuta, akayamimina kichwani pake, akambusu, akasema, Je! BWANA hakukutia mafuta [uwe mkuu juu ya watu wake Israeli? Nawe utamiliki watu wa BWANA, na kuwaokoa kutoka kwa mikono ya adui zao; kisha hii itakuwa ishara kwako ya kuwa BWANA amekutia mafuta] uwe mkuu juu ya urithi wake.


Basi sasa, nakusihi, bwana wangu, mfalme, na asikie maneno ya mtumishi wake. Ikiwa ni BWANA aliyekuchochea juu yangu, na akubali sadaka; bali ikiwa ni wanadamu, na walaaniwe mbele za BWANA; kwa sababu wamenifukuza leo, nisishikamane na urithi wa BWANA, wakisema, Nenda, ukatumikie miungu mingine.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo