Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Samueli 19:8 - Swahili Revised Union Version

8 Ndipo mfalme akaondoka, akaketi langoni. Nao wote wakaambiwa ya kwamba, Angalieni, mfalme ameketi langoni; watu wote wakaenda huko mbele ya mfalme. Basi, Israeli wote walikuwa wamekimbia kila mtu hemani kwake.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Kisha, mfalme akatoka akaenda, akaketi mahali pake karibu na lango. Watu wote walipoambiwa kuwa mfalme yuko langoni, wote walimwendea. Wakati huo, watu wote wa Israeli walikuwa wamekimbia, kila mmoja nyumbani kwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Kisha, mfalme akatoka akaenda, akaketi mahali pake karibu na lango. Watu wote walipoambiwa kuwa mfalme yuko langoni, wote walimwendea. Wakati huo, watu wote wa Israeli walikuwa wamekimbia, kila mmoja nyumbani kwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Kisha, mfalme akatoka akaenda, akaketi mahali pake karibu na lango. Watu wote walipoambiwa kuwa mfalme yuko langoni, wote walimwendea. Wakati huo, watu wote wa Israeli walikuwa wamekimbia, kila mmoja nyumbani kwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Kwa hiyo, mfalme akaondoka na kuketi kwenye kiti chake langoni. Watu walipoambiwa, “Mfalme ameketi langoni,” watu wote wakamjia. Wakati huo, Waisraeli walikuwa wamekimbilia nyumbani mwao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Kwa hiyo mfalme akaondoka akaketi kitini pake penye lango. Watu walipoambiwa, “Mfalme ameketi langoni,” watu wote wakamjia. Wakati huo, Waisraeli walikuwa wamekimbilia nyumbani kwao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Ndipo mfalme akaondoka, akaketi langoni. Nao wote wakaambiwa ya kwamba, Angalieni, mfalme ameketi langoni; watu wote wakaenda huko mbele ya mfalme. Basi, Israeli wote walikuwa wamekimbia kila mtu hemani kwake.

Tazama sura Nakili

2 Samueli 19:8
10 Marejeleo ya Msalaba  

Tena Absalomu huondoka asubuhi na mapema, na kusimama kando ya njia ya lango; kisha ikawa, mtu yeyote aliyekuwa na neno, lililokuwa halina budi kufika kwa mfalme ili kuhukumiwa, Absalomu humwita mtu huyo kwake, na kumwuliza, Wewe u mtu wa mji gani? Naye akasema, Mtumishi wako ni mtu wa kabila fulani ya Israeli.

Nao wakamtwaa Absalomu wakamtupa katika shimo kubwa mle msituni, wakaweka juu yake rundo kubwa sana la mawe; kisha Israeli wote wakakimbia kila mtu hemani mwake.

Basi Daudi alikuwa ameketi kati ya malango mawili; mlinzi akapanda juu hata dari ya lile lango hata ukutani, akainua macho yake, akaangalia, na tazama, mtu anakuja mbio peke yake.

Mfalme akawaambia, Yaliyo mema machoni penu ndiyo nitakayofanya. Basi mfalme akasimama kando ya lango, na hao watu wakatoka kwa maeelfu yao na mamia yao.

Watu wakajificha siku ile, wakaingia mjini kama vile watu waonao fedheha wajifichavyo, hapo wakimbiapo vitani.

Ikapigwa mbiu jeshini, jua likichwa, kusema, Kila mtu aende mjini kwake, na kila mtu shambani kwake.

Yuda wakashindwa mbele ya Israeli; wakakimbia kila mtu hemani kwake.

Basi akaenda Yehoramu mpaka Sairi, na magari yake yote pamoja naye. Akaondoka usiku, akawapiga Waedomi waliomzunguka yeye na makamanda wa magari; na watu wakakimbilia hemani kwao.

Wafilisti wakapigana nao, Israeli wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana katika Israeli walianguka watu elfu thelathini walioenda vitani kwa miguu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo