Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Samueli 19:21 - Swahili Revised Union Version

21 Lakini Abishai, mwana wa Seruya, akajibu na kusema, Je! Shimei hatauawa kwa sababu hii, kwa kuwa amemlaani masihi wa BWANA?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Ndipo Abishai mwana wa Seruya akasema, “Je, si lazima Shimei auawe maana alimlaani mtu ambaye Mwenyezi-Mungu amemteua kwa kumpaka mafuta?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Ndipo Abishai mwana wa Seruya akasema, “Je, si lazima Shimei auawe maana alimlaani mtu ambaye Mwenyezi-Mungu amemteua kwa kumpaka mafuta?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Ndipo Abishai mwana wa Seruya akasema, “Je, si lazima Shimei auawe maana alimlaani mtu ambaye Mwenyezi-Mungu amemteua kwa kumpaka mafuta?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Ndipo Abishai mwana wa Seruya akasema, “Je, Shimei hapaswi kuuawa kwa ajili ya hili? Alimlaani mpakwa mafuta wa Mwenyezi Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Ndipo Abishai mwana wa Seruya akasema, “Je, Shimei hapaswi kuuawa kwa ajili ya hili? Alimlaani mpakwa mafuta wa bwana.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

21 Lakini Abishai, mwana wa Seruya, akajibu na kusema, Je! Shimei hatauawa kwa sababu hii, kwa kuwa amemlaani masihi wa BWANA?

Tazama sura Nakili

2 Samueli 19:21
10 Marejeleo ya Msalaba  

Basi wakaendelea njiani Daudi na watu wake; Shimei naye akaaendelea juu ya ubavu wa kile kilima, kwa kumkabili, huku akiendelea, akilaani, akimtupia mawe, na kurusha mavumbi.

Basi mfalme Daudi alipofika Bahurimu, tazama, kulitoka huko mtu wa jamaa ya nyumba ya Sauli, jina lake akiitwa Shimei, mwana wa Gera; alitoka, akalaani alipokuwa akienda.

Ndipo Abishai mwana wa Seruya, akamwambia mfalme, Mbona mbwa mfu huyu amlaani mfalme bwana wangu? Na nivuke, nakusihi, nikaondoe kichwa chake.

Ee Mungu, ngao yetu, uangalie, Umtazame uso masihi

Usimtukane Mungu, wala usimlaani mkuu wa watu wako.

Pumzi ya mianzi ya pua zetu, masihi wa BWANA, Alikamatwa katika marima yao; Ambaye kwa habari zake tulisema, Chini ya kivuli chake tutakaa kati ya mataifa.

Akawaambia watu wake, Hasha! Nisimtendee bwana wangu, masihi wa BWANA, neno hili, kuunyosha mkono wangu juu yake, kwa maana yeye ni masihi wa BWANA.

Lakini Daudi akamwambia Abishai, Usimwangamize; kwani ni nani awezaye kuunyosha mkono wake juu ya masihi wa BWANA, naye akawa hana hatia?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo