Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

2 Samueli 16:11 - Swahili Revised Union Version

11 Daudi akamwambia Abishai, na watumishi wake wote, Angalieni, huyu mwanangu, aliyetoka viunoni mwangu, anautafuta uhai wangu; sembuse Mbenyamini huyu? Mwacheni alaani, kwa sababu BWANA ndiye aliyemwagiza.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Tena mfalme Daudi akamwambia Abishai na hata watumishi wake wote, “Ikiwa mtoto wangu mwenyewe anayawinda maisha yangu, je si zaidi mtu wa kabila la Benyamini? Nyinyi mwacheni anilaani kwani Mwenyezi-Mungu amemwagiza anilaani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Tena mfalme Daudi akamwambia Abishai na hata watumishi wake wote, “Ikiwa mtoto wangu mwenyewe anayawinda maisha yangu, je si zaidi mtu wa kabila la Benyamini? Nyinyi mwacheni anilaani kwani Mwenyezi-Mungu amemwagiza anilaani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Tena mfalme Daudi akamwambia Abishai na hata watumishi wake wote, “Ikiwa mtoto wangu mwenyewe anayawinda maisha yangu, je si zaidi mtu wa kabila la Benyamini? Nyinyi mwacheni anilaani kwani Mwenyezi-Mungu amemwagiza anilaani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Ndipo Daudi akamwambia Abishai na maafisa wake wote, “Mwanangu, ambaye ametoka viunoni mwangu mwenyewe, anajaribu kuniua. Je, si zaidi sana huyu Mbenyamini! Mwacheni; acha alaani, kwa maana Mwenyezi Mungu amemwambia afanye hivyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Ndipo Daudi akamwambia Abishai na maafisa wake wote, “Mwanangu, yeye ambaye ametoka viunoni mwangu mwenyewe, anajaribu kuuondoa uhai wangu. Je, si zaidi sana kwa huyu Mbenyamini! Mwacheni, acha alaani, kwa maana bwana amemwambia afanye hivyo.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Daudi akamwambia Abishai, na watumishi wake wote, Angalieni, huyu mwanangu, aliyetoka viunoni mwangu, anautafuta uhai wangu; sembuse Mbenyamini huyu? Mwacheni alaani, kwa sababu BWANA ndiye aliyemwagiza.

Tazama sura Nakili

2 Samueli 16:11
14 Marejeleo ya Msalaba  

Nalo neno la BWANA likamjia likinena, Huyu hatakurithi, bali utakayemzaa ndiye atakayekurithi.

Basi sasa, msihuzunike, wala msiudhike nafsi zenu, kwa kuniuza huku; maana Mungu alinituma mbele yenu kuhifadhi maisha ya watu.

Basi ilitukia ya kwamba kulikuwapo mtu asiyefaa, jina lake akiitwa Sheba, mwana wa Bikri, Mbenyamini; naye akapiga tarumbeta, akasema, Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni kila mtu hemani kwake, enyi Israeli.

mfalme akamwambia Nathani, nabii, Angalia sasa, mimi ninakaa katika nyumba ya mierezi, bali sanduku la Mungu linakaa ndani ya mapazia.

Ikawa, alipokuwa akiabudu nyumbani mwa Nisroki, mungu wake, Adrameleki na Shareza wakampiga kwa upanga; wakaikimbilia nchi ya Ararati. Na Esar-hadoni mwanawe akatawala mahali pake.

Naye BWANA akatuma malaika aliyewakatia mbali wapiganaji vita wote, na majemadari, na makamanda, kambini mwa mfalme wa Ashuru. Basi akarudia nchi yake kwa aibu. Naye alipoingia nyumbani mwa mungu wake, baadhi ya wanawe mwenyewe wakamwangamiza humo kwa upanga.

Waache walaani, bali Wewe utabariki, Wanaonishambulia na waaibishwe, Naye mtumishi wako afurahi.

Na nabii akidanganyika, na kusema neno, mimi, BWANA, nimemdanganya nabii yule, nami nitaunyosha mkono wangu juu yake, na kumwangamiza, asiwe kati ya watu wangu Israeli.

Tena niliwapa amri zisizokuwa njema, na hukumu ambazo hawakuweza kuishi kwazo;

Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao, na kuwaua.

Basi sasa, nakusihi, bwana wangu, mfalme, na asikie maneno ya mtumishi wake. Ikiwa ni BWANA aliyekuchochea juu yangu, na akubali sadaka; bali ikiwa ni wanadamu, na walaaniwe mbele za BWANA; kwa sababu wamenifukuza leo, nisishikamane na urithi wa BWANA, wakisema, Nenda, ukatumikie miungu mingine.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo