Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Yohana 5:14 - Swahili Revised Union Version

14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya matakwa yake, yeye hutusikiliza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya matakwa yake, yeye hutusikiliza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Na sisi tuko thabiti mbele ya Mungu kwani tuna hakika kwamba tukimwomba chochote kadiri ya matakwa yake, yeye hutusikiliza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mungu, kwamba tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mwenyezi Mungu, kwamba kama tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 5:14
26 Marejeleo ya Msalaba  

basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.


Hata wakafanya kilio cha maskini kumfikia, Naye akasikia kilio cha hao wateswao.


Hutimiza matakwa ya wote wamchao, Na pia husikia kilio chao, na huwaokoa.


Nami nilisema kwa pupa yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya kilio changu Wakati nilipokulilia.


Walilia, naye BWANA akasikia, Akawaponya kutoka kwa taabu zao zote.


Kwa kuwa BWANA huwasikia wahitaji, Wala hawadharau wafungwa wake.


Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia; Na wenye haki watapewa matakwa yao.


BWANA yuko mbali na wasio haki; Bali huisikia sala ya mwenye haki.


Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.


Na yoyote mtakayoyaomba katika sala mkiamini, mtapokea.


Nami nilijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nilisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.


Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.


Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo nanyi mtatendewa.


Hata sasa hamjaomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu.


Tunajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.


Katika yeye tunao ujasiri na uwezo wa kukaribia katika tumaini kwa njia ya kumwamini.


Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu.


Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;


bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya tumaini letu mpaka mwisho.


Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.


Basi ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, ili mpate kuponywa. Sala yake mwenye haki ina nguvu nyingi, na hutenda mengi.


Na sasa, watoto wadogo, kaeni ndani yake, ili kusudi, atakapofunuliwa, muwe na ujasiri, wala msiaibike mbele zake katika kuja kwake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo