Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Yohana 3:14 - Swahili Revised Union Version

14 Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana tunawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Sisi tunajua kwamba tumekwisha pita kutoka katika kifo na kuingia katika uhai kwa sababu tunawapenda ndugu zetu. Mtu asiye na upendo hubaki katika kifo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Sisi tunajua kwamba tumekwisha pita kutoka katika kifo na kuingia katika uhai kwa sababu tunawapenda ndugu zetu. Mtu asiye na upendo hubaki katika kifo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Sisi tunajua kwamba tumekwisha pita kutoka katika kifo na kuingia katika uhai kwa sababu tunawapenda ndugu zetu. Mtu asiye na upendo hubaki katika kifo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Sisi tunajua kwamba tumepita mautini kuingia uzimani, kwa sababu tunawapenda ndugu. Kila asiyempenda ndugu yake akaa mautini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Sisi tunajua ya kwamba tumepita mautini kuingia uzimani, kwa sababu tunawapenda ndugu. Kila asiyempenda ndugu yake akaa mautini.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana tunawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti.

Tazama sura Nakili




1 Yohana 3:14
31 Marejeleo ya Msalaba  

Nao watakatifu waliopo duniani, ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.


Mtu aikosaye njia ya busara Atakaa katika mkutano wao waliokufa.


Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.


kwa kuwa huyu mwanangu alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana. Wakaanza kushangilia.


Bali ilibidi kusherehekea na kushangilia kwa kuwa huyu ndugu yako alikuwa amekufa, naye amefufuka; alikuwa amepotea, naye ameonekana.


maana, analipenda taifa letu, naye alitujengea sinagogi.


Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.


Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi.


Haya nawaamuru ninyi, mpate kupendana.


Amin, amin, nawaambia, Yeye alisikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenituma ana uzima wa milele; wala haingii hukumuni, bali amepita kutoka mautini kuingia uzimani.


Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni.


Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,


Kwa sababu hiyo mimi nami, tangu nilipopata habari za imani yenu katika Bwana Yesu, na pendo lenu kwa watakatifu wote,


Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;


hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alitufanya kuwa hai pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.


tangu tuliposikia habari za imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo mlio nao kwa watakatifu wote;


Kuhusu upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana.


Upendano wa ndugu na udumu.


Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo safi.


Neno la mwisho ni hili; muwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu;


na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.


Na katika hili tunajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake.


Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri.


Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.


Nimewaandikia ninyi mambo hayo, ili mjue ya kuwa mna uzima wa milele, ninyi mnaoliamini Jina la Mwana wa Mungu.


Katika hili tunajua kwamba tunawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo