Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 8:16 - Swahili Revised Union Version

16 Tokea siku ile nilipowatoa watu wangu Israeli katika Misri, sikuchagua mji wowote katika kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe hapo; lakini nilimchagua Daudi awe juu ya watu wangu Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 ‘Tangu niwaondoe watu wangu Israeli nchini Misri, sikuchagua mji wowote katika makabila ya Israeli ili nijengewe nyumba nitakamoabudiwa; ila nilimchagua Daudi, atawale watu wangu, Israeli.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 ‘Tangu niwaondoe watu wangu Israeli nchini Misri, sikuchagua mji wowote katika makabila ya Israeli ili nijengewe nyumba nitakamoabudiwa; ila nilimchagua Daudi, atawale watu wangu, Israeli.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 ‘Tangu niwaondoe watu wangu Israeli nchini Misri, sikuchagua mji wowote katika makabila ya Israeli ili nijengewe nyumba nitakamoabudiwa; ila nilimchagua Daudi, atawale watu wangu, Israeli.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 ‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu Israeli kutoka Misri, sikuchagua mji katika kabila lolote la Israeli ili Hekalu lijengwe humo na Jina langu liwe humo, bali nimemchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 ‘Tangu siku niliyowatoa watu wangu Israeli kutoka Misri, sikuchagua mji katika kabila lolote la Israeli ili Hekalu lijengwe humo ili Jina langu lipate kuwamo humo, bali nimemchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.’

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

16 Tokea siku ile nilipowatoa watu wangu Israeli katika Misri, sikuchagua mji wowote katika kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe hapo; lakini nilimchagua Daudi awe juu ya watu wangu Israeli.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 8:16
17 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko.


Macho yako yafumbuke na kuielekea nyumba hii usiku na mchana, mahali hapa ulipopataja, ukasema, Hapa ndipo litakapokuwapo jina langu; ili uyasikie maombi ya mtumwa wako aombapo akikabili mahali hapa.


BWANA akasema Nitawahamisha Yuda pia mbali nami, kama nilivyowahamisha Israeli, nami nitautupa mji huu niliouchagua, naam, Yerusalemu, na nyumba ile niliyoinena, Jina langu litakuwa humo.


Ikawa usiku uo huo, neno la Mungu likamjia Nathani, kusema,


Walakini BWANA, Mungu wa Israeli, alinichagua katika nyumba yote ya babangu kuwa mfalme juu ya Israeli milele, kwa kuwa amemchagua Yuda awe mkuu; na katika nyumba ya Yuda, alichagua nyumba ya babangu, na miongoni mwa wana wa babangu, aliniridhia mimi ili kunitawaza niwe mfalme juu ya Israeli wote;


bali mkinirudia mimi, na kuzishika amri zangu na kuzitenda, watu wako waliofukuzwa wajapokuwa katika pande za mwisho za mbingu, hata hivyo nitawakusanya kutoka huko, na kuwaleta mpaka mahali pale nilipopachagua ili kuliweka jina langu hapo.


Kwa kuwa BWANA ameichagua Sayuni, Ameitamani akae ndani yake.


Akamchagua Daudi, mtumishi wake, Akamwondoa katika mazizi ya kondoo.


Nimefanya agano na mteule wangu, Nimemuapia Daudi, mtumishi wangu.


Lakini nendeni sasa hadi mahali pangu palipokuwapo katika Shilo, nilipolikalisha jina langu hapo kwanza, mkaone nilivyopatenda kwa sababu ya uovu wa watu wangu Israeli.


wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA.


Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika makabila yenu yote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe uende huko;


BWANA akamwambia Samweli, utamlilia Sauli hadi lini, kwa kuwa mimi nimemkataa asiwatawale Waisraeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakutuma kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo