Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 8:15 - Swahili Revised Union Version

15 Akasema, BWANA, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenena na Daudi baba yangu kwa kinywa chake akalitimiza kwa mkono wake, akasema,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 akasema, “Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kwani kwa nguvu yake ametimiza ahadi yake aliyompa baba yangu Daudi, akisema:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 akasema, “Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kwani kwa nguvu yake ametimiza ahadi yake aliyompa baba yangu Daudi, akisema:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 akasema, “Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kwani kwa nguvu yake ametimiza ahadi yake aliyompa baba yangu Daudi, akisema:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Kisha akasema: “Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ambaye kwa mkono wake mwenyewe ametimiza alilomwahidi Daudi baba yangu kwa kinywa chake mwenyewe. Kwa kuwa alisema,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Kisha akasema: “Ahimidiwe bwana, Mungu wa Israeli, ambaye kwa mkono wake mwenyewe ametimiza lile alilomwahidi Daudi baba yangu kwa kinywa chake mwenyewe. Kwa kuwa alisema,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Akasema, BWANA, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenena na Daudi baba yangu kwa kinywa chake akalitimiza kwa mkono wake, akasema,

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 8:15
29 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha Daudi alipokwisha kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani akawabariki watu kwa jina la BWANA wa majeshi.


Basi sasa, Ee BWANA Mungu, neno lile ulilolinena kuhusu mtumishi wako, na kuhusu nyumba yangu, uliimarishe milele, ukatende kama ulivyosema.


Nenda, ukamwambie mtumishi wangu, Daudi, BWANA asema hivi, Je! Wewe utanijengea nyumba, nikae ndani yake?


Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, tangu milele hata milele. Na watu wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA.


Yeye ndiye atakayenijengea nyumba, nami nitakiimarisha kiti cha enzi cha ufalme wake milele.


huyo ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya jina langu; naye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa babaye; nami nitakiimarisha milele kiti cha ufalme wake juu ya Israeli.


Kwa hiyo Daudi akamhimidi BWANA, mbele ya mkutano wote; naye Daudi akasema, Uhimidiwe, Ee BWANA, Mungu wa Israeli baba yetu, milele na milele.


Ndipo Daudi akawaambia kusanyiko lote, Haya, mhimidini BWANA, Mungu wenu. Basi kusanyiko lote wakamhimidi BWANA, Mungu wa baba zao, wakainamisha vichwa vyao, wakamsujudia BWANA, na mfalme naye.


Hata siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka; maana ndipo walipomtukuza BWANA; kwa hiyo jina lake mahali pale pakaitwa Bonde la Baraka hata leo.


Akasema, BWANA, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenena kwa kinywa chake na baba yangu Daudi, akalitimiza kwa mikono yake, akasema,


Ndipo Walawi, Yeshua na Kadmieli, na Bani, na Hashabneya, na Sherebia, na Hodia, na Shebania, na Pethahia, wakasema, Simameni, mkamhimidi BWANA, Mungu wenu, tangu milele na hata milele. Na lihimidiwe jina lako tukufu, lililotukuka kuliko baraka zote na sifa zote.


Bali sisi tutamhimidi BWANA, Tangu leo na hata milele.


Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako, na jina lako juu ya vyote.


Na atukuzwe BWANA, Mungu wa Israeli, Tangu milele hata milele. Amina na Amina.


bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha BWANA kimenena haya.


Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.


Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli, Kwa kuwa amewajia watu wake, na kuwakomboa.


Kama alivyosema tangu mwanzo Kwa kinywa cha manabii wake watakatifu;


Ili kuwatendea rehema baba zetu, Na kulikumbuka agano lake takatifu;


Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;


Halikuanguka neno lolote katika jambo lolote lililokuwa ni jema ambalo BWANA alikuwa amelinena katika habari ya nyumba ya Israeli; yalitimia mambo yote.


Ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu;


Naye Daudi akamwambia Abigaili, Na ahimidiwe BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye amekuleta hivi leo kunilaki;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo