Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 21:25 - Swahili Revised Union Version

25 (Lakini hapakuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza atende maovu machoni pa BWANA ambaye Yezebeli mkewe alimchochea.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 (Hakuna mtu aliyenuia kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu kama Ahabu, ambaye alishawishiwa na Yezebeli, mkewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 (Hakuna mtu aliyenuia kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu kama Ahabu, ambaye alishawishiwa na Yezebeli, mkewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 (Hakuna mtu aliyenuia kutenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu kama Ahabu, ambaye alishawishiwa na Yezebeli, mkewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 (Hapajapata kamwe kuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza mwenyewe kutenda uovu machoni pa Mwenyezi Mungu, akiwa anachochewa na Yezebeli mkewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 (Hapajapata kamwe kuwa na mtu kama Ahabu, aliyejiuza mwenyewe kutenda uovu machoni mwa bwana, akiwa anachochewa na Yezebeli mkewe.

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 21:25
26 Marejeleo ya Msalaba  

Omri akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akatenda maovu kuliko wote waliomtangulia;


Naye akajibu, Si mimi niliyewataabisha Israeli; bali ni wewe, na nyumba ya baba yako, kwa kuwa mmeziacha amri za BWANA; nawe umewafuata mabaali.


kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, Obadia akatwaa manabii mia moja, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji).


Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao.


Ahabu akamwambia Eliya, Je! Umenipata, ewe adui yangu? Akamwambia, Nimekupata, kwa sababu umejiuza utende yaliyo mabaya machoni pa BWANA.


Yezebeli mkewe akamwambia, Je! Sasa wewe unaumiliki ufalme wa Israeli? Ondoka, ule chakula, moyo wako ufurahi; mimi nitakupa shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli.


Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akaiendea njia ya babaye, na njia ya mamaye, na njia ya Yeroboamu mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli.


Akamtumikia Baali, akamwabudu, akamghadhibisha BWANA, Mungu wa Israeli, kwa mfano wa mambo yote aliyoyafanya baba yake.


Wakawapitisha watoto wao, wa kiume na wa kike, motoni, wakapiga ramli, wakafanya uchawi, wakajiuza wenyewe wapate kufanya yaliyo maovu machoni pa BWANA, hata kumkasirisha.


Kabla ya huyo hapakuwa na mfalme mfano wake, aliyemwelekea BWANA kwa moyo wake wote, na kwa roho yake yote, na kwa nguvu zake zote, sawasawa na Sheria ya Musa; wala baada yake hakuinuka mmoja mfano wake yeye.


Ikawa, Yoramu alipomwona Yehu, akasema, Je! Ni amani, Yehu? Akajibu, Amani gani, maadamu uzinzi wa mama yako Yezebeli na uchawi wake ni mwingi?


Alipoingia, akala, na kunywa; kisha akasema, Haya! Mwangalieni mwanamke huyu aliyelaaniwa, mkamzike; kwa maana ni binti mfalme.


Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; lakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.


Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao.


Kinywa cha malaya ni shimo refu; Anayechukiwa na BWANA atatumbukia ndani yake.


Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye.


BWANA asema hivi, Iko wapi hati ya talaka ya mama yenu, ambayo kwa hiyo niliachana naye? Au nimewauza ninyi kwa nani katika watu wanaoniwia? Ninyi mliuzwa kwa sababu ya maovu yenu; tena mama yenu ameachwa kwa sababu ya makosa yenu.


Maana BWANA asema hivi, Mliuzwa bure; nanyi mtakombolewa bila fedha.


Lakini Wayahudi wasioamini wakawataharakisha watu wa Mataifa na kuwatia nia mbaya juu ya ndugu.


Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.


Nasema kwa jinsi ya kibinadamu kwa sababu ya udhaifu wa miili yenu. Kwa kuwa kama mlivyovitoa viungo vyenu vitumiwe na uchafu na uasi mpate kuasi, vivyo hivyo sasa vitoeni viungo vyenu vitumiwe na haki mpate kutakaswa.


Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi.


Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule mwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo