Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Wafalme 2:42 - Swahili Revised Union Version

42 Basi, mfalme akatuma watu, akamwita Shimei, akamwambia, Je! Sikukuapisha kwa BWANA, na kukushuhudia, kusema, Siku ile utakapotoka ukaenda mahali popote, ujue kwamba hakika utakufa? Nawe ukaniambia, Neno hili nililolisikia ni jema?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

42 alimwita Shimei na kumwambia, “Je, hukuniapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu kwamba hutatoka Yerusalemu, nami sikukuonya kwa dhati kwamba, hakika utakufa kama utathubutu kwenda nje? Nawe ulikubali, ukaniambia, ‘Vema, nitatii.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

42 alimwita Shimei na kumwambia, “Je, hukuniapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu kwamba hutatoka Yerusalemu, nami sikukuonya kwa dhati kwamba, hakika utakufa kama utathubutu kwenda nje? Nawe ulikubali, ukaniambia, ‘Vema, nitatii.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

42 alimwita Shimei na kumwambia, “Je, hukuniapia kwa jina la Mwenyezi-Mungu kwamba hutatoka Yerusalemu, nami sikukuonya kwa dhati kwamba, hakika utakufa kama utathubutu kwenda nje? Nawe ulikubali, ukaniambia, ‘Vema, nitatii.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

42 mfalme akamwita Shimei na kumwambia, “Je, sikukuapiza kwa Mwenyezi Mungu na kukuonya kuwa, ‘Siku utakayoondoka kwenda mahali pengine popote, uwe na hakika utakufa’? Wakati ule uliniambia, ‘Ulilolisema ni jema. Nitatii!’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

42 mfalme akamwita Shimei na kumwambia, “Je, sikukuapiza kwa bwana na kukuonya kuwa, ‘Siku utakayoondoka kwenda mahali pengine popote, uwe na hakika utakufa?’ Wakati ule uliniambia, ‘Ulilolisema ni jema. Nitatii!’

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

42 Basi, mfalme akatuma watu, akamwita Shimei, akamwambia, Je! Sikukuapisha kwa BWANA, na kukushuhudia, kusema, Siku ile utakapotoka ukaenda mahali popote, ujue kwamba hakika utakufa? Nawe ukaniambia, Neno hili nililolisikia ni jema?

Tazama sura Nakili

1 Wafalme 2:42
6 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Sulemani akaambiwa, ya kwamba Shimei alikuwa ametoka Yerusalemu kwenda Gathi, na kurudi tena.

Mbona basi hukukishika kiapo chako kwa BWANA, na amri niliyokuagiza?

Anayedharau waovu Machoni pake, Bali huwaheshimu wamchao BWANA Aliyeapa ingawa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake.

Lakini baba aliwaambia watumwa wake, Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike; mtieni na pete kidoleni, na viatu miguuni;

Akamwambia, Nitakuhukumu kwa kinywa chako, mtumwa mwovu wewe. Ulinijua kuwa ni mtu mgumu, nichukuaye nisichoweka, na kuvuna nisichopanda;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo