Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Wafalme 2:3 - Swahili Revised Union Version

3 uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Timiza maagizo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ufuate njia zake na kushika masharti yake, amri zake, hukumu zake na kuheshimu maamuzi yake kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, ili upate kufanikiwa katika kila ufanyalo na kokote uendako, pia

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Timiza maagizo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ufuate njia zake na kushika masharti yake, amri zake, hukumu zake na kuheshimu maamuzi yake kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, ili upate kufanikiwa katika kila ufanyalo na kokote uendako, pia

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Timiza maagizo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ufuate njia zake na kushika masharti yake, amri zake, hukumu zake na kuheshimu maamuzi yake kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, ili upate kufanikiwa katika kila ufanyalo na kokote uendako, pia

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 shika lile Mwenyezi Mungu, Mungu wako, analokuagiza: Nenda katika njia zake, ushike maagizo na amri zake, sheria zake na kanuni zake, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, ili upate kustawi katika yote ufanyayo na popote utakapoenda,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 shika lile bwana Mwenyezi Mungu wako analokuagiza: Enenda katika njia zake, ushike maagizo na amri zake, sheria zake na kanuni zake, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, ili upate kustawi katika yote ufanyayo na popote uendako,

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;

Tazama sura Nakili




1 Wafalme 2:3
33 Marejeleo ya Msalaba  

Akaweka askari wenye kulinda ngome katika Edomu; katikati ya Edomu yote akaweka ngome, na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye BWANA akampa Daudi ushindi kila kokote alikokwenda.


Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumishi wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye BWANA akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.


Sulemani naye akampenda BWANA, akienda katika amri za Daudi babaye, ila hutoa dhabihu na kufukiza uvumba katika mahali pa juu.


Naye BWANA akawa pamoja naye, kila alikokwenda alifanikiwa; tena alimwasi mfalme wa Ashuru, wala hakumtumikia.


naye Sulemani mwanangu, umjalie ili kwa moyo wote, azishike amri zako, na shuhuda zako, na maagizo yako, akayatende hayo yote na kuijenga nyumba hii ya enzi, niliyoiwekea akiba.


Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele, Maana ndizo changamko la moyo wangu.


Umeziagiza shuhuda zako kwa haki, Na kwa uaminifu mwingi.


Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote.


Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia hekima mtu asiye nayo.


Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.


Nanyi mtakaa mlangoni pa hema ya kukutania muda wa siku saba mchana na usiku, na kuulinda ulinzi wa BWANA ili kwamba msife; kwani ndivyo nilivyoagizwa.


Ikumbukeni Torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.


tukaitwaa nchi yao, nayo tukawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila la Manase, iwe urithi.


Shikeni basi maneno ya agano hili myafanye, ili mfanikiwe katika yote mfanyayo.


Na sasa, Ee Israeli, zisikilizeni amri na hukumu ninazowafundisha, ili mzitende; mpate kuishi na kuingia na kuimiliki nchi anayowapa BWANA, Mungu wa baba zenu.


haya ndiyo maagizo, amri na hukumu, Musa alizowaambia wana wa Israeli walipotoka Misri;


Angalieni nimewafundisha amri na hukumu, vile vile kama BWANA, Mungu wangu, alivyoniamuru, ili mzitende katika nchi mwingiayo ili kuimiliki.


Tena liko taifa gani kubwa, lililo na amri na hukumu zenye haki kama torati hii yote, ninayoiweka mbele yenu leo?


Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu nisemazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuzizingatia.


Lakini mjibidiishe sana kuzifanya amri na sheria, ambazo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwaamuru, kumpenda BWANA, Mungu wenu, na kwenenda katika njia zake zote, na kuzishika amri zake, na kushikamana na yeye, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na nafsi yenu yote.


Basi, iweni thabiti sana kuyashika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati ya Musa, na kuyatenda, msiyaache kwa kugeukia upande wa kulia wala upande wa kushoto.


Naye Daudi akatenda kwa busara katika njia zake zote naye BWANA alikuwa pamoja naye.


Wakati huo wakuu wa Wafilisti wakatokeza; kisha ikawa, kila mara walipotokeza, Daudi alipata ushindi zaidi kuliko watumishi wote wa Sauli hivyo jina lake likawa na sifa kuu.


Basi Daudi akatoka kwenda kila mahali alikotumwa na Sauli, akatenda kwa akili; Sauli akamweka juu ya watu wa vita; jambo hili likawa jema machoni pa watu wote, na machoni pa watumishi wa Sauli pia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo