Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Wafalme 1:53 - Swahili Revised Union Version

53 Basi mfalme Sulemani akatuma watu, wakamteremsha toka madhabahuni. Naye akaja, akamwinamia mfalme Sulemani; naye Sulemani akamwambia, Nenda nyumbani kwako.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

53 Basi, mfalme Solomoni akaagiza Adoniya aitwe kutoka hemani, aje kwake. Adoniya akafika mbele ya mfalme, akainama kwa heshima. Mfalme akamwambia, “Nenda zako nyumbani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

53 Basi, mfalme Solomoni akaagiza Adoniya aitwe kutoka hemani, aje kwake. Adoniya akafika mbele ya mfalme, akainama kwa heshima. Mfalme akamwambia, “Nenda zako nyumbani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

53 Basi, mfalme Solomoni akaagiza Adoniya aitwe kutoka hemani, aje kwake. Adoniya akafika mbele ya mfalme, akainama kwa heshima. Mfalme akamwambia, “Nenda zako nyumbani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

53 Ndipo Mfalme Sulemani akawatuma watu, nao wakamshusha kutoka madhabahuni. Naye Adoniya akaja akamwinamia Mfalme Sulemani, naye Sulemani akamwambia, “Nenda nyumbani mwako.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

53 Ndipo Mfalme Sulemani akawatuma watu, nao wakamshusha kutoka madhabahuni. Naye Adoniya akaja akamwinamia Mfalme Sulemani, naye Sulemani akamwambia, “Nenda nyumbani kwako.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

53 Basi mfalme Sulemani akatuma watu, wakamteremsha toka madhabahuni. Naye akaja, akamwinamia mfalme Sulemani; naye Sulemani akamwambia, Nenda nyumbani kwako.

Tazama sura Nakili

1 Wafalme 1:53
10 Marejeleo ya Msalaba  

hata siku ya tatu ikawa, tazama! Akaja mtu kutoka kambi ya Sauli, nguo zake zimeraruliwa, tena ana mavumbi kichwani mwake; basi, ikawa alipomfikia Daudi, akaanguka chini, akamsujudia.

Naye mfalme akasema, Ageukie nyumbani kwake, asinione uso wangu. Basi Absalomu akarejea nyumbani kwake, asimwone uso mfalme.

Absalomu akakaa miaka miwili mizima katika Yerusalemu; asimwone uso mfalme.

Basi Yoabu akamwendea mfalme, akamwambia hayo, naye alipomwita Absalomu, yeye akaja kwa mfalme, akainama kifudifudi hadi chini mbele ya mfalme; naye mfalme akambusu Absalomu.

Bathsheba akainama, akamsujudia mfalme. Naye mfalme akamwuliza, Wataka nini?

Ndipo Bathsheba akainama kifudifudi, akamsujudia mfalme, akasema, Bwana wangu mfalme Daudi na aishi milele.

Sulemani Akasema, Akionekana kuwa mtu wa kweli, hata unywele wake mmoja hautaanguka chini; lakini uovu ukionekana ndani yake, atakufa.

Basi siku ya kufa kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe, akasema,

Tena, mfalme akatuma watu akamwita Shimei, akamwambia, Ujijengee nyumba humu Yerusalemu, ukae ndani yake, wala usitoke humo kwenda mahali popote.

Mwanangu, mche BWANA, na mfalme; Wala usishirikiane na wenye kigeugeu;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo