Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Samueli 9:24 - Swahili Revised Union Version

24 Basi mpishi akatwaa paja, na nyama iliyokuwa juu yake, akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, Iliyowekwa kando ndiyo hiyo! Iweke mbele yako ule, kwa sababu umewekewa hiyo wewe hadi wakati uliokusudiwa, maana nilisema, Nimewaalika watu. Basi Sauli akala pamoja na Samweli siku hiyo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Yule mpishi akaenda akaleta paja na sehemu ya nyama iliyokuwa upande wa juu wa paja hilo na kuviweka mbele ya Shauli. Ndipo Samueli akamwambia Shauli, “Tazama kile ulichowekewa; sasa kimewekwa mbele yako. Sasa ule kwa sababu kimewekwa kwa ajili yako ili upate kula pamoja na wageni.” Hivyo, Shauli akala pamoja na Samueli siku hiyo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Yule mpishi akaenda akaleta paja na sehemu ya nyama iliyokuwa upande wa juu wa paja hilo na kuviweka mbele ya Shauli. Ndipo Samueli akamwambia Shauli, “Tazama kile ulichowekewa; sasa kimewekwa mbele yako. Sasa ule kwa sababu kimewekwa kwa ajili yako ili upate kula pamoja na wageni.” Hivyo, Shauli akala pamoja na Samueli siku hiyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Hivyo mpishi akachukua mguu pamoja na kile kilichokuwa juu yake akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, “Hiki ndicho ambacho kimewekwa kwa ajili yako. Ule, kwa sababu kilitengwa kwa ajili yako kwa tukio hili, tangu niliposema, ‘Nimewaalika wageni.’ ” Naye Sauli akala pamoja na Samweli siku ile.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

BIBLIA KISWAHILI

24 Basi mpishi akatwaa paja, na nyama iliyokuwa juu yake, akaiweka mbele ya Sauli. Samweli akasema, Iliyowekwa kando ndiyo hiyo! Iweke mbele yako ule, kwa sababu umewekewa hiyo wewe hadi wakati uliokusudiwa, maana nilisema, Nimewaalika watu. Basi Sauli akala pamoja na Samweli siku hiyo.

Tazama sura Nakili

1 Samueli 9:24
6 Marejeleo ya Msalaba  

Tena yatwae mafuta ya huyo kondoo dume, na mkia wake wa mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo katika hizo figo, na paja la kulia; kwani ni kondoo ambaye ni wa kuwekwa kwa kazi takatifu;

Nawe kitakase kile kidari cha ile sadaka ya kutikiswa, na lile paja la sadaka ya kuinuliwa, lililotikiswa, na lililoinuliwa juu, vya yule kondoo wa kuwekwa kwa kazi takatifu, huyo aliyekuwa kwa ajili ya Haruni, na huyo aliyekuwa kwa ajili ya wanawe;

vikusanye vipande vyake ndani yake, naam, kila kipande chema, paja na bega; lijaze mifupa iliyochaguliwa.

Tena nyama yao itakuwa ni yako wewe, kama kile kidari cha kutikiswa, na kama mguu wa nyuma wa upande wa kulia, itakuwa yako.

Samweli akamwambia mpishi, Lete ile sehemu niliyokupa, hiyo niliyokuambia, Iweke kando.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo