Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Samueli 6:9 - Swahili Revised Union Version

9 Kisha angalieni, likikwea kwa njia ya mpakani mwake kwenda Beth-shemeshi, basi, ndiye aliyetutenda uovu huo mkuu; la, sivyo, ndipo tutakapojua ya kwamba si mkono wake uliotupiga; ilikuwa ni bahati mbaya iliyotupata.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Bali angalieni, ikiwa gari hilo linakwenda moja kwa moja kuelekea nchi yake yaani kwenye mji wa Beth-shemeshi, basi, hapo tutajua kuwa aliyetuletea tauni hii ni Mungu wa Israeli. Lakini kama haliendi huko, basi, tutajua kuwa sio mkono wake uliotupiga, bali maafa haya yametupata kwa bahati mbaya.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Bali angalieni, ikiwa gari hilo linakwenda moja kwa moja kuelekea nchi yake yaani kwenye mji wa Beth-shemeshi, basi, hapo tutajua kuwa aliyetuletea tauni hii ni Mungu wa Israeli. Lakini kama haliendi huko, basi, tutajua kuwa sio mkono wake uliotupiga, bali maafa haya yametupata kwa bahati mbaya.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 lakini liangalieni kwa makini. Iwapo litaenda katika nchi yake lenyewe, kuelekea Beth-Shemeshi, basi tutajua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye alileta haya maafa makubwa juu yetu. Lakini kama halikwenda, basi tutajua kwamba haukuwa mkono wa Mwenyezi Mungu uliotupiga na kwamba iliyotokea kwetu ni ajali.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 lakini liangalieni kwa makini. Iwapo litakwenda katika nchi yake lenyewe, kuelekea Beth-Shemeshi, basi tutajua kwamba bwana ndiye alileta haya maafa makubwa juu yetu. Lakini kama halikwenda, basi tutajua kwamba haukuwa mkono wa bwana uliotupiga na kwamba iliyotokea kwetu ni ajali.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Kisha angalieni, likikwea kwa njia ya mpakani mwake kwenda Beth-shemeshi, basi, ndiye aliyetutenda uovu huo mkuu; la, sivyo, ndipo tutakapojua ya kwamba si mkono wake uliotupiga; ilikuwa ni bahati mbaya iliyotupata.

Tazama sura Nakili

1 Samueli 6:9
13 Marejeleo ya Msalaba  

Yule kijana aliyempa habari akasema, Nilikuwapo kwa nasibu juu ya kilima cha Gilboa, na tazama, Sauli alikuwa ameegemea fumo lake; na tazama, magari na wapanda farasi wanamfuatia kwa kasi.

Mwana wa Dekari, kutoka Makasi, na Shaalbimu na Beth-shemeshi na Elon-beth-hanani.

Basi Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea; wakatazamana uso kwa uso, yeye na Amazia mfalme wa Yuda huko Beth-shemeshi, ulio wa Yuda.

Lakini Farao alipoona ya kuwa pana nafuu, akaufanya moyo wake kuwa mzito, asiwasikize; kama BWANA alivyonena.

Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba si wenye mbio washindao katika michezo, wala si walio hodari washindao vitani, wala si wenye hekima wapatao chakula, wala si watu wa ufahamu wapatao mali, wala wenye ustadi wapatao upendeleo; lakini wakati na bahati huwapata wote.

BWANA, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.

Je! Tarumbeta itapigwa mjini, watu wasiogope? Mji utapatikana na hali mbaya, asiyoileta BWANA?

Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipita kando.

kisha mpaka ukazunguka kutoka Baala kwendelea upande wa magharibi hadi kilima Seiri, kisha ukaendelea hadi upande wa mlima wa Yearimu upande wa kaskazini (huo ndio Kesaloni), kisha ukateremkia Beth-shemeshi, na kwendelea karibu na Timna;

na Aini, pamoja na mbuga zake za malisho, na Yuta pamoja na mbuga zake za malisho, na Beth-shemeshi pamoja na mbuga zake za malisho; miji tisa katika makabila hayo mawili.

Basi watu wale walifanya hivyo; wakatwaa ng'ombe wawili wakamuliwao, wakawafunga garini, na ndama wao wakawafunga zizini;

Na hao ng'ombe wakashika njia moja kwa moja kwenda Beth-shemeshi; wakaiandama njia ya barabara, wakaenda wakilia, lakini hawakugeukia upande wa kulia wala wa kushoto; na wakuu wa Wafilisti wakawafuata hata kuufikia mpaka wa Beth-shemeshi.

Nao wakajibu, Mkilirudisha hilo sanduku la Mungu wa Israeli, msilirudishe kitupu; lakini msikose kumpelekea na matoleo ya kosa; hivyo mtapona, tena mtafunuliwa ni kwa sababu gani mkono wake haukuondolewa kwenu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo