Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Samueli 30:24 - Swahili Revised Union Version

24 Tena ni nani atakayewasikiliza ninyi katika jambo hili? Kwa kuwa kama lilivyo fungu lake yeye ashukaye vitani, ndivyo litakavyokuwa na fungu lake huyo akaaye karibu na vyombo; watagawiwa sawasawa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Hakuna mtu atakayekubaliana na mawazo yenu! Yule aliyekwenda vitani na yule aliyebaki na mizigo yetu, kila mtu atapewa sehemu inayolingana na mwenzake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Hakuna mtu atakayekubaliana na mawazo yenu! Yule aliyekwenda vitani na yule aliyebaki na mizigo yetu, kila mtu atapewa sehemu inayolingana na mwenzake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Hakuna mtu atakayekubaliana na mawazo yenu! Yule aliyekwenda vitani na yule aliyebaki na mizigo yetu, kila mtu atapewa sehemu inayolingana na mwenzake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Ni nani atasikiliza yale mnayosema? Fungu la mtu aliyekaa na vyombo litakuwa sawa na la yule aliyeenda vitani. Wote watashiriki sawa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Ni nani atasikiliza yale mnayosema? Fungu la mtu aliyekaa na vyombo litakuwa sawa na la yule aliyekwenda vitani. Wote watashiriki sawa.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

24 Tena ni nani atakayewasikiliza ninyi katika jambo hili? Kwa kuwa kama lilivyo fungu lake yeye ashukaye vitani, ndivyo litakavyokuwa na fungu lake huyo akaaye karibu na vyombo; watagawiwa sawasawa.

Tazama sura Nakili

1 Samueli 30:24
7 Marejeleo ya Msalaba  

Wafalme wa majeshi wanakimbia, wanakimbia; Na mwanamke akaaye nyumbani anagawa nyara.

ukagawanye nyara katika mafungu mawili; kati ya wanajeshi waliotoka nje kupigana vita na hio jumuiya nzima;

kisha akanena nao, na kuwaambia, Rudini na mali mengi mahemani kwenu, na ng'ombe wengi sana, na fedha, na dhahabu, na shaba, na chuma, na mavazi mengi sana; mgawane na ndugu zenu hizo nyara za adui zenu.

Na kila mtu aliyekuwa katika hali ya dhiki, na kila mtu aliyekuwa na deni, na watu wote wenye uchungu mioyoni mwao, wakakusanyika kwake; naye akawa jemadari wao; nao waliokuwa pamoja naye walikuwa kama watu mia nne.

Kisha Daudi akawaambia watu wake, Haya! Jifungeni kila mtu upanga wake. Nao wakajifunga kila mtu upanga wake; Daudi naye akajifunga upanga wake; nao wakapanda nyuma yake Daudi, wakiwa kama watu mia nne; na watu mia mbili wakakaa na vyombo vyao.

Ndipo Daudi akasema, La, ndugu zangu, msitende hivyo katika hizo nyara alizotupa BWANA, ambaye ndiye aliyetuhifadhi, akalitia mikononi mwetu lile jeshi lililokuja kinyume chetu.

Basi ikawa hivyo tangu siku ile na baadaye; akaiweka iwe amri na agizo la Israeli hata leo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo