Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

1 Samueli 21:2 - Swahili Revised Union Version

2 Daudi akamwambia Ahimeleki, kuhani, Mfalme ameniagiza shughuli, akaniambia, Asijue mtu awaye yote habari ya shughuli hii ninayokutuma, wala ya neno hili ninalokuamuru; nami nimewaagiza vijana waende mahali fulani.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Daudi akamjibu, “Niko hapa kutokana na amri ya mfalme. Aliniambia nisimweleze mtu yeyote juu ya kile ambacho amenituma. Nimeagana na watu wangu kwamba tukutane mahali fulani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Daudi akamjibu, “Niko hapa kutokana na amri ya mfalme. Aliniambia nisimweleze mtu yeyote juu ya kile ambacho amenituma. Nimeagana na watu wangu kwamba tukutane mahali fulani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Daudi akamjibu, “Niko hapa kutokana na amri ya mfalme. Aliniambia nisimweleze mtu yeyote juu ya kile ambacho amenituma. Nimeagana na watu wangu kwamba tukutane mahali fulani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, akisema, “Mfalme ameniagiza shughuli fulani na kuniambia, ‘Mtu yeyote asijue chochote kuhusu kazi niliyokutuma kuifanya, wala maagizo niliyokupa!’ Kuhusu watu wangu, nimewaambia mahali pa kukutana.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, akisema, “Mfalme ameniagiza shughuli fulani na kuniambia, ‘Mtu yeyote asijue chochote kuhusu kazi yako wala maagizo yako!’ Kuhusu watu wangu, nimewaambia tukutane mahali fulani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Daudi akamwambia Ahimeleki, kuhani, Mfalme ameniagiza shughuli, akaniambia, Asijue mtu awaye yote habari ya shughuli hii ninayokutuma, wala ya neno hili ninalokuamuru; nami nimewaagiza vijana waende mahali fulani.

Tazama sura Nakili

1 Samueli 21:2
13 Marejeleo ya Msalaba  

Isaka akamwuliza mwanawe, Imekuwaje umepata upesi namna hii, mwanangu? Akasema, Kwa sababu BWANA, Mungu wako, amenifanikisha.

Akamwuliza, Wewe ndiwe kweli mwanangu Esau? Akasema, Ndimi.

Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la BWANA, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.

Anathothi, Nobu, Anania;

Uniondolee njia ya uongo, Unineemeshe kwa sheria yako.

Ee BWANA, uweke mlinzi kinywani pangu, Mngojezi mlangoni pa midomo yangu.

siku hii ya leo atasimama huko Nobu; anatikisa mkono wake juu ya mlima wa binti Sayuni, mlima wa Yerusalemu.

Kwa maana kabla hawajaja watu kadhaa waliotoka kwa Yakobo, alikuwa akila pamoja na watu wa Mataifa; lakini hao walipokuja, akarudi nyuma akajitenga, huku akiwaogopa waliotahiriwa.

Msiambiane uongo, kwa kuwa mmevua kabisa utu wa kale, pamoja na matendo yake;

Sauli akamwambia Mikali, Mbona wewe umenidanganya hivi, na kumwacha adui yangu aende, hata ameniponyoka? Naye Mikali akamjibu Sauli, Yeye aliniambia, Niache niende zangu; kwa nini nikuue?

Kuna nini basi, chini ya mkono wako? Nipe mkononi mwangu mikate mitano, au chochote ulicho nacho hapa.

Daudi akamwambia Abiathari, Siku ile alipokuwako Doegi, Mwedomi, nilijua hakika ya kuwa atamwambia Sauli; mimi nimewapatia watu wote wa jamaa ya baba yako kifo.

Ndipo akajibu Doegi, Mwedomi, aliyesimama karibu na watumishi wa Sauli, akasema, Mimi nilimwona mwana wa Yese akienda Nobu, kwa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo