Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Samueli 15:24 - Swahili Revised Union Version

24 Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeivunja amri ya BWANA, pia na maneno yako; kwa sababu niliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Shauli akamwambia Samueli, “Nimetenda dhambi. Nimeasi amri ya Mwenyezi-Mungu na amri yako, kwa sababu niliwaogopa watu, nikawatii wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Shauli akamwambia Samueli, “Nimetenda dhambi. Nimeasi amri ya Mwenyezi-Mungu na amri yako, kwa sababu niliwaogopa watu, nikawatii wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Shauli akamwambia Samueli, “Nimetenda dhambi. Nimeasi amri ya Mwenyezi-Mungu na amri yako, kwa sababu niliwaogopa watu, nikawatii wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Ndipo Sauli akamwambia Samweli, “Nimetenda dhambi. Nimevunja amri ya Mwenyezi Mungu na maagizo yako. Niliwaogopa watu na kwa hiyo nikafanya walivyotaka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Ndipo Sauli akamwambia Samweli, “Nimetenda dhambi. Nimevunja amri ya bwana na maagizo yako. Niliwaogopa watu na kwa hiyo nikafanya walivyotaka.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

24 Ndipo Sauli akamwambia Samweli, Nimefanya dhambi; maana nimeivunja amri ya BWANA, pia na maneno yako; kwa sababu niliwaogopa wale watu, nikaitii sauti yao.

Tazama sura Nakili




1 Samueli 15:24
21 Marejeleo ya Msalaba  

Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.


Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako;


Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi. Nathani akamwambia Daudi, BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa.


Kwa sababu niliwaogopa mkutano mkubwa, Na dharau la jamaa lilinitia hofu, Hata nilinyamaa kimya, nisitoke mlangoni.


Nimekutenda dhambi Wewe peke yako, Na kufanya maovu mbele za macho yako. Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo, Na kuwa safi utoapo hukumu.


Ndipo Farao akawaita Musa na Haruni haraka; akasema, Nimemfanyia dhambi BWANA, Mungu wenu na ninyi pia.


Usiwafuate walio wengi kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotoa hukumu;


Farao akatuma watu, na kuwaita Musa na Haruni, na kuwaambia, Mimi nimekosa wakati huu; BWANA ni mwenye haki, na mimi na watu wangu tu waovu.


Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.


Naye mfalme Sedekia akasema, Tazama, yuko mikononi mwenu; maana mfalme siye awezaye kufanya neno lolote kinyume chenu.


Balaamu akamwambia malaika wa BWANA, Nimefanya dhambi; maana sikujua ya kuwa wewe umesimama njiani ili kunipinga; basi sasa, ikiwa umechukizwa, nitarudi tena.


Wakasema, Basi, haya yatuhusu nini sisi? Yaangalie haya wewe mwenyewe.


Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.


Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa.


Akasema, Nimekosa; lakini uniheshimu sasa, nakuomba, mbele ya wazee wa watu wangu, na mbele ya Israeli, rudi pamoja nami, nimwabudu BWANA, Mungu wako.


Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng'ombe, na vinono, na wana-kondoo, na chochote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali chochote kilichokuwa kibaya na kisichofaa, ndicho walichoangamiza kabisa.


Kwa nini basi mnaipiga teke dhabihu yangu na sadaka yangu nilizoziamuru katika maskani yangu; ukawaheshimu wanao kuliko mimi, mpate kujinenepesha kwa sadaka zote za watu wangu Israeli zilizo njema?


Ndipo Sauli akasema, Nimekosa; rudi, Daudi, mwanangu; maana sitakudhuru tena, kwa kuwa maisha yangu yalikuwa na thamani machoni pako leo; angalia, nimetenda upumbavu, nimekosa sana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo