Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Wafilipi 1:26 - Neno: Maandiko Matakatifu

26 Ili kwamba furaha yenu iwe nyingi katika Al-Masihi Isa kwa ajili yangu kwa kule kuja kwangu kwenu tena.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Basi, nitakapokuwa nanyi tena mtakuwa na sababu ya kuona fahari juu yangu katika kuungana na Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Basi, nitakapokuwa nanyi tena mtakuwa na sababu ya kuona fahari juu yangu katika kuungana na Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Basi, nitakapokuwa nanyi tena mtakuwa na sababu ya kuona fahari juu yangu katika kuungana na Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 ili kwa kuja kwangu kwenu tena, furaha yenu iwe nyingi katika Al-Masihi Isa kwa ajili yangu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 hata mzidi kuona fahari katika Kristo Yesu juu yangu kwa sababu ya kuwapo kwangu pamoja nanyi tena.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

26 Basi, nitakapokuwa nanyi tena mtakuwa na sababu ya kuona fahari juu yangu katika kuungana na Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 1:26
14 Marejeleo ya Msalaba  

Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu, bibi arusi wangu; nimekusanya manemane yangu pamoja na kikolezo changu. Nimekula sega langu la asali na asali yangu; nimekunywa divai yangu na maziwa yangu. Kuleni, enyi marafiki, mnywe; kunyweni ya kutosha, ee wapenzi.


Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi na furaha yenu hakuna awaondoleaye.


Mpaka sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili.


kama vile mlivyotuelewa kwa sehemu, mtakuja kuelewa kwa ukamilifu ili mweze kujivuna kwa ajili yetu, kama na sisi tutakavyojivuna kwa ajili yenu katika siku ya Bwana Isa.


Sio kwamba tunajaribu kujistahilisha kwenu tena, lakini tunataka kuwapa nafasi ili mwone fahari juu yetu mweze kuwajibu hao wanaoona fahari juu ya mambo yanayoonekana badala ya mambo yaliyo moyoni.


Nilikuwa nimewasifu ninyi kwake, nanyi hamkuniaibisha. Lakini kila kitu tulichowaambia ninyi, kilikuwa kweli, hivyo kule kujisifu kwetu kwa Tito kuwahusu ninyi kumethibitishwa kuwa kweli pia.


Mara nyingi najivuna kwa ajili yenu; naona fahari juu yenu. Nimejawa na faraja. Nina furaha kupita kiasi katika mateso yetu yote.


Bali Mungu, yeye awafarijie wenye huzuni, alitufariji kwa kufika kwake Tito.


Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo aweze kujisifu, bila kujilinganisha na mtu mwingine.


Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika Bwana Isa! Mimi kuwaandikia mambo yale yale hakuniudhi, kwa maana ni kinga kwa ajili yenu.


Kwa maana sisi ndio tulio tohara, sisi tumwabuduo Mwenyezi Mungu katika Roho, tunaona fahari katika Al-Masihi Isa, ambao hatuweki tumaini letu katika mwili,


Nina furaha kubwa katika Bwana Isa kwamba hatimaye mmeanza upya kushughulika tena na maisha yangu. Kweli mmekuwa mkinifikiria lakini mlikuwa hamjapata nafasi ya kufanya hivyo.


Furahini katika Bwana Isa siku zote, tena nasema furahini!


Tufuate:

Matangazo


Matangazo