Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Wafilipi 1:26 - Biblia Habari Njema

26 Basi, nitakapokuwa nanyi tena mtakuwa na sababu ya kuona fahari juu yangu katika kuungana na Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema - BHND

26 Basi, nitakapokuwa nanyi tena mtakuwa na sababu ya kuona fahari juu yangu katika kuungana na Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Basi, nitakapokuwa nanyi tena mtakuwa na sababu ya kuona fahari juu yangu katika kuungana na Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 ili kwa kuja kwangu kwenu tena, furaha yenu iwe nyingi katika Al-Masihi Isa kwa ajili yangu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Ili kwamba furaha yenu iwe nyingi katika Al-Masihi Isa kwa ajili yangu kwa kule kuja kwangu kwenu tena.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 hata mzidi kuona fahari katika Kristo Yesu juu yangu kwa sababu ya kuwapo kwangu pamoja nanyi tena.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

26 Basi, nitakapokuwa nanyi tena mtakuwa na sababu ya kuona fahari juu yangu katika kuungana na Kristo Yesu.

Tazama sura Nakili




Wafilipi 1:26
14 Marejeleo ya Msalaba  

Naingia bustanini mwangu, dada yangu, bi arusi. Nakusanya manemane na viungo, nala sega langu la asali, nanywa divai yangu na maziwa yangu. Kuleni enyi marafiki, kunyweni; kunyweni sana wapendwa wangu.


Nyinyi pia mna huzuni sasa; lakini nitawajieni tena, nanyi mtajaa furaha mioyoni mwenu, na furaha hiyo hakuna mtu atakayeiondoa kwenu.


Mpaka sasa hamjaomba chochote kwa jina langu. Ombeni nanyi mtapata ili furaha yenu ikamilike.


maana mpaka sasa mmenielewa kiasi fulani tu. Tunajua kwamba katika ile siku ya Bwana Yesu mtaweza kutuonea sisi fahari kama nasi tunavyowaonea nyinyi fahari.


Si kwamba tunajaribu tena kujipendekeza kwenu, ila tunataka kuwapa nyinyi sababu zetu za kuona fahari juu yenu, ili mpate kuwajibu wale wanaojivunia hali yao ya nje zaidi kuliko jinsi walivyo moyoni.


Mimi nimewasifu sana mbele yake, na katika jambo hilo sikudanganyika. Tumewaambieni ukweli daima, na kule kuwasifia nyinyi mbele ya Tito kumekuwa jambo la ukweli tupu.


Nina imani kubwa sana ninaposema nanyi; naona fahari kubwa juu yenu! Katika taabu zetu nimepata kitulizo kikubwa na kufurahi mno.


Lakini Mungu, mwenye kuwapa shime wanyonge, alitupa moyo sisi pia kwa kuja kwake Tito.


Lakini kila mmoja na aupime vizuri mwenendo wake mwenyewe. Ukiwa mwema, basi, anaweza kuona fahari juu ya alichofanya bila kuwa na sababu ya kujilinganisha na mtu mwingine.


Hatimaye, ndugu zangu, furahini katika kuungana na Bwana. Sichoki kurudia yale niliyokwisha andika pale awali, maana yatawaongezeeni usalama.


Watu waliotahiriwa kikweli ni sisi, si wao; kwani sisi twamwabudu Mungu kwa njia ya Roho wake, na kuona fahari katika kuungana na Kristo Yesu. Mambo ya nje tu hatuyathamini.


Katika kuungana na Bwana nimepata furaha kubwa kwamba mwishoni mlipata tena fursa ya kuonesha kwamba mnanikumbuka. Kusema kweli mmekuwa mkinikumbuka daima ila tu hamkupata nafasi ya kuonesha jambo hilo.


Basi, furahini daima katika kuungana na Bwana! Nasema tena: Furahini!


Tufuate:

Matangazo


Matangazo