Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 7:7 - Neno: Maandiko Matakatifu

7 “Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni mlango, nanyi mtafunguliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni mlango, nanyi mtafunguliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni mlango, nanyi mtafunguliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 “Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa;

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

7 “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata; bisheni mlango, nanyi mtafunguliwa.

Tazama sura Nakili




Mathayo 7:7
43 Marejeleo ya Msalaba  

Siku hiyo watumishi wa Isaka wakaja wakampa habari kuhusu kisima walichokuwa wamekichimba, wakamwambia, “Tumepata maji!”


bwana akamtokea Sulemani huko Gibeoni wakati wa usiku katika ndoto, naye Mungu akasema, “Omba lolote utakalo nikupe.”


Unasikia, Ee bwana, shauku ya wanaoonewa, wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao,


Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu, katika mawazo yake yote hakuna nafasi ya Mungu.


Sifa ni zako, Ee bwana, nifundishe maagizo yako.


Moyo wangu unasema kuhusu wewe, “Utafute uso wake!” Uso wako, bwana “Nitautafuta.”


Nilimtafuta bwana naye akanijibu, akaniokoa kwenye hofu zangu zote.


Jifurahishe katika bwana naye atakupa haja za moyo wako.


na uniite siku ya taabu; nami nitakuokoa, nawe utanitukuza.”


Maskini wataona na kufurahi: ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi!


Lakini wote wakutafutao washangilie na kukufurahia, wale wapendao wokovu wako siku zote waseme, “Mungu na atukuzwe!”


Ee bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe, umejaa upendo kwa wote wakuitao.


Nawapenda wale wanipendao, na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.


Sasa nitaondoka na kuzunguka mjini, katika barabara zake na viwanja; nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye. Kwa hiyo nilimtafuta lakini sikumpata.


Enyi watu wa Sayuni, mnaoishi Yerusalemu, hamtalia tena. Tazameni jinsi atakavyokuwa na huruma mtakapolia kwa kumwomba msaada! Mara asikiapo, atawajibu.


‘Niite nami nitakuitika na kukuambia mambo makuu na yasiyochunguzika, usiyoyajua.’


Hili ndilo bwana asemalo kwa nyumba ya Israeli: “Nitafuteni mpate kuishi;


“Tena nawaambia, ikiwa wawili wenu watakubaliana duniani kuhusu jambo lolote watakaloomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.


Yoyote mtakayoyaomba mkisali na mkiamini, mtayapokea.”


Lakini utafuteni kwanza Ufalme wa Mwenyezi Mungu na haki yake, na haya yote atawapa pia.


Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?


Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango.


Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote mtakayoyaomba mkisali, aminini ya kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu.


Wakati mwenye nyumba atakapoondoka na kufunga mlango, mtasimama nje mkibisha mlango na kusema, ‘Bwana! Tufungulie mlango!’ “Lakini yeye atawajibu, ‘Siwajui ninyi, wala mtokako.’


Kisha Isa akawapa wanafunzi wake mfano ili kuwaonyesha kuwa yawapasa kuomba pasipo kukata tamaa.


Si ninyi mlionichagua, bali mimi ndiye niliyewachagua ninyi na kuwaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kudumu. Ili nalo lolote mtakalomwomba Baba katika Jina langu, awape ninyi.


Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtatendewa.


Isa akajibu akamwambia, “Kama ungelijua karama ya Mungu, naye ni nani anayekuambia, Nipe maji ninywe, wewe ungelimwomba yeye, naye angelikupa maji yaliyo hai.”


Wale ambao kwa kuvumilia katika kutenda mema hutafuta utukufu, heshima na maisha yasiyoharibika, Mungu atawapa uzima wa milele.


Hakuna hata mmoja mwenye ufahamu, hakuna hata mmoja amtafutaye Mungu.


Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana yeyote anayemjia Mwenyezi Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.


Kule kuomba kwa imani kutamwokoa huyo mgonjwa, naye Bwana Isa atamwinua, na kama ametenda dhambi, atasamehewa.


lolote tuombalo, twalipokea kutoka kwake, kwa sababu tumezitii amri zake na kutenda yale yanayompendeza.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo