Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 5:4 - Neno: Maandiko Matakatifu

4 Heri wale wanaohuzunika, maana hao watafarijiwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Heri wale wanaohuzunika, maana hao watafarijiwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

4 Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.

Tazama sura Nakili




Mathayo 5:4
34 Marejeleo ya Msalaba  

Katika siku ile utasema: “Nitakusifu wewe, Ee bwana. Ingawa ulinikasirikia, hasira yako imegeukia mbali nawe umenifariji.


yeye atameza mauti milele. bwana Mwenyezi atafuta machozi katika nyuso zote; ataondoa aibu ya watu wake duniani kote. bwana amesema hili.


Enyi watu wa Sayuni, mnaoishi Yerusalemu, hamtalia tena. Tazameni jinsi atakavyokuwa na huruma mtakapolia kwa kumwomba msaada! Mara asikiapo, atawajibu.


waliokombolewa na bwana watarudi. Wataingia Sayuni wakiimba; furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao. Watapata furaha na shangwe; huzuni na majonzi vitakimbia.


Nimeziona njia zake, lakini nitamponya, nitamwongoza na kumrudishia upya faraja,


“Shangilieni pamoja na Yerusalemu na mfurahi kwa ajili yake, ninyi nyote mnaompenda, shangilieni kwa nguvu pamoja naye, ninyi nyote mnaoomboleza juu yake.


Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote, hivyo vikapata kuwepo?” asema bwana. “Mtu huyu ndiye ninayemthamini: yeye ambaye ni mnyenyekevu na mwenye roho yenye toba, atetemekaye asikiapo neno langu.


Wale wote watakaopona na kutoroka watakuwa milimani, wakiomboleza kama hua wa mabondeni, kila mmoja kwa sababu ya dhambi zake.


akamwambia, “Pita katika mji wote wa Yerusalemu ukaweke alama juu ya vipaji vya nyuso za wale watu wanaohuzunika na kuomboleza kwa sababu ya machukizo yote yanayotendeka katika mji huu.”


“Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.


“Lakini Ibrahimu akamjibu, ‘Mwanangu, kumbuka kwamba wakati wa uhai wako ulipata mambo mazuri, lakini Lazaro alipata mambo mabaya. Lakini sasa anafarijiwa hapa na wewe uko katika maumivu makuu.


Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa sababu mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mnaolia sasa, kwa sababu mtacheka.


Ole wenu ninyi mlioshiba sasa, maana mtaona njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, maana mtaomboleza na kulia.


Yule mwanamke akasimama nyuma ya miguu ya Isa akilia. Akailowanisha miguu yake kwa machozi yake, kisha akaifuta kwa nywele zake, akaibusu na kuimiminia manukato.


Isa akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.”


Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji la uzima Mwenyezi Mungu alilowaahidia wale wampendao.


Atafuta kila chozi kutoka macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”


Tufuate:

Matangazo


Matangazo