Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mathayo 5:3 - Neno: Maandiko Matakatifu

3 “Heri walio maskini wa roho, maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 “Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 “Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 “Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 “Heri walio maskini wa roho, maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

3 “Heri walio maskini rohoni, maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Tazama sura Nakili




Mathayo 5:3
55 Marejeleo ya Msalaba  

Katika dhiki yake akamsihi bwana Mwenyezi Mungu wake na kujinyenyekeza sana mbele za Mungu wa baba zake.


Maombi yake, pamoja na jinsi Mungu alivyoguswa na kusihi kwake, pia dhambi zake zote na kukosa kwake uaminifu pamoja na sehemu alizojenga mahali pa juu pa kuabudia miungu, kule kusimamisha nguzo za Ashera na sanamu kabla ya kujinyenyekeza kwake, yote yameandikwa katika kumbukumbu za waonaji.


Lakini tofauti na Manase baba yake, hakujinyenyekeza mbele za bwana, badala yake Amoni aliongeza hatia zaidi na zaidi.


Kwa kuwa moyo wako ulikuwa msikivu na ulijinyenyekeza mbele za Mungu uliposikia kile nilichosema dhidi ya mahali hapa na watu wake na kwa sababu ulijinyenyekeza mbele zangu na uliyararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nimekusikia, asema bwana.


kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao.


Kwa hiyo najidharau mwenyewe, na kutubu katika mavumbi na majivu.”


Heri mtu yule ambaye haendi katika shauri la watu waovu, wala hasimami katika njia ya wenye dhambi, au kuketi katika baraza la wenye mizaha.


Msifuni bwana. Heri mtu yule amchaye bwana, mtu yule apendezwaye sana na amri zake.


Heri ni wale wote wamchao bwana, waendao katika njia zake.


Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake, ambaye tumaini lake ni katika bwana, Mungu wake,


Mbusu Mwana, asije akakasirika nawe ukaangamizwa katika njia yako, kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula. Heri wote wanaomkimbilia.


bwana yu karibu na waliovunjika moyo, na huwaokoa waliopondeka roho.


Heri mtu yule anayemjali mnyonge, bwana atamwokoa wakati wa shida.


Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika, moyo uliovunjika wenye toba, Ee Mungu, hutaudharau.


Ee bwana Mwenye Nguvu Zote, heri ni mtu yule anayekutumaini wewe.


Ni afadhali kuwa mnyenyekevu katika roho miongoni mwa walioonewa kuliko kugawana nyara pamoja na wenye kiburi.


Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima.


“Basi sasa wanangu, nisikilizeni; heri wale wanaozishika njia zangu.


Hata hivyo bwana anatamani kutupatia neema, anainuka ili kuwaonyesha huruma. Kwa kuwa bwana ni Mungu wa haki. Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!


Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu, yeye aliyeinuliwa sana, yeye aishiye milele, ambaye jina lake ni Mtakatifu: “Ninaishi mimi mahali palipoinuka na patakatifu, lakini pia pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na mwenye roho ya unyenyekevu, ili kuzihuisha roho za wanyenyekevu na kuihuisha mioyo yao waliotubu.


Roho wa bwana Mwenyezi yu juu yangu, kwa sababu bwana amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao;


Je, mkono wangu haukufanya vitu hivi vyote, hivyo vikapata kuwepo?” asema bwana. “Mtu huyu ndiye ninayemthamini: yeye ambaye ni mnyenyekevu na mwenye roho yenye toba, atetemekaye asikiapo neno langu.


Amekuonyesha yaliyo mema, ee mwanadamu. bwana anataka nini kwako? Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.


Wakati huo Isa alisema, “Nakuhimidi Baba, Mwenyezi Mungu, Bwana wa mbingu na nchi, kwa kuwa umewaficha mambo haya wenye hekima na wenye elimu, nawe ukawafunulia watoto wadogo.


Amebarikiwa mtu yule asiyechukizwa na mimi.”


Lakini heri macho yenu kwa sababu yanaona, na heri masikio yenu kwa sababu yanasikia.


Isa akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mbinguni ni wa wale walio kama hawa.”


Heri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo.


“Ndipo Mfalme atawaambia wale walioko upande wake wa kuume, ‘Njooni, ninyi mliobarikiwa na Baba yangu; urithini Ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuumbwa kwa ulimwengu.


“Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni umekaribia.”


Ninawaambia kwamba wengi watatoka mashariki na magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Ibrahimu, Isaka na Yakobo katika Ufalme wa Mbinguni.


Isa alipoona yaliyokuwa yakitukia, akachukizwa. Akawaambia wanafunzi wake, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana Ufalme wa Mwenyezi Mungu ni wa wale walio kama hawa.


Isa akajibu, “Wamebarikiwa zaidi wale wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”


“Nawaambia, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu zaidi ya yule Farisayo. Kwa maana yeyote ajikwezaye atashushwa, na yeyote ajishushaye atakwezwa.”


Nami kama Baba yangu alivyonipa ufalme, kadhalika mimi nami ninawapa ninyi,


ili mpate kula na kunywa mezani pangu katika karamu ya ufalme wangu, na kukaa katika viti vya enzi, mkihukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.”


“Roho wa Mwenyezi Mungu yu juu yangu, kwa sababu amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru wanaoonewa,


Isa akamwambia, “Umeamini kwa kuwa umeniona? Wamebarikiwa wale ambao hawajaona lakini wameamini.”


Kumbuka jinsi bwana Mwenyezi Mungu wenu alivyowaongoza katika njia yote katika jangwa kwa miaka hii arobaini, kukunyenyekeza na kukujaribu ili ajue lililoko moyoni mwako, kwamba utayashika maagizo yake au la.


Lakini yeye aliye tajiri afurahi kwa kuwa ameshushwa, kwa sababu atatoweka kama ua la shambani.


Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji la uzima Mwenyezi Mungu alilowaahidia wale wampendao.


Ndugu zangu, sikilizeni: Je, Mwenyezi Mungu hakuwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu kuwa matajiri katika imani na kuurithi Ufalme aliowaahidi wale wampendao?


Ndipo malaika akaniambia, “Andika: ‘Wamebarikiwa wale walioalikwa kwenye karamu ya arusi ya Mwana-Kondoo!’ ” Naye akaongeza kusema, “Haya ndiyo maneno ya kweli ya Mungu.”


“Wamebarikiwa wale wafuao mavazi yao, ili wapate haki ya kuuendea huo mti wa uzima na kuuingia huo mji kupitia kwenye malango yake.


Kwa maana unasema: ‘Mimi ni tajiri, nimejilimbikizia mali, wala sihitaji kitu chochote.’ Lakini hutambui ya kwamba wewe ni mnyonge, wa kuhurumiwa, maskini, kipofu, tena uliye uchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo