Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Danieli 12:3 - Neno: Maandiko Matakatifu

3 Wale wenye hekima watang’aa kama mwanga wa mbingu, nao wale ambao huwaongoza wengi kutenda haki, watang’aa kama nyota milele na milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Wale wenye hekima watangaa kama anga angavu, na wale waliowaongoza wengine kutenda mema, watangaa kama nyota milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Wale wenye hekima watangaa kama anga angavu, na wale waliowaongoza wengine kutenda mema, watangaa kama nyota milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Wale wenye hekima watang'aa kama anga angavu, na wale waliowaongoza wengine kutenda mema, watang'aa kama nyota milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Wale wenye hekima watang’aa kama mwanga wa mbingu, nao wale ambao huwaongoza wengi kutenda haki, watang’aa kama nyota milele na milele.

Tazama sura Nakili

Swahili Roehl Bible 1937

3 Ndipo, wafunzi watakapoangaza kama mwangaza wa mbinguni, nao walioongoza wengi, wapate wongofu, wataangaza kama nyota kale na kale zamani zote.

Tazama sura Nakili

Swahili Revised Union Version

3 Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.

Tazama sura Nakili




Danieli 12:3
27 Marejeleo ya Msalaba  

waliona kuwa uso wake unang’aa. Kisha Musa angeliweka tena utaji juu ya uso wake mpaka alipokwenda kuzungumza na bwana.


Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima, naye mwenye hekima huvuta roho za watu.


Wenye hekima hurithi heshima, bali huwaaibisha wapumbavu.


Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko, ambayo hung’aa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu.


Mhubiri hakuwa tu na hekima, bali aliwagawia watu maarifa pia. Alitafakari na kutafiti na akaweka katika utaratibu mithali nyingi.


Baada ya maumivu ya nafsi yake, ataona nuru ya uzima na kuridhika; kwa maarifa yake, mtumishi wangu mwenye haki atawafanya wengi kuwa wenye haki, naye atayachukua maovu yao.


Lakini kama wangesimama barazani mwangu, wangetangaza maneno yangu kwa watu wangu, nao wangewageuza kutoka njia zao mbaya na kutoka matendo yao maovu.”


“Wenye hekima watawafundisha wengi, ingawa kwa kitambo watauawa kwa upanga au kuchomwa moto, au kukamatwa au kufanywa mateka.


Baadhi ya wenye hekima watajikwaa, ili waweze kusafishwa, kutakaswa na kufanywa wasio na waa mpaka wakati wa mwisho, kwa maana bado litakuja kwa wakati ulioamriwa.


Wengi watatakaswa, na kuondolewa mawaa na kufanywa safi, lakini waovu wataendelea kuwa waovu. Hakuna mmoja wa waovu atakayefahamu, lakini wale wenye hekima watafahamu.


Ndipo wenye haki watang’aa kama jua katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu, Baba yao. Yeye aliye na masikio, na asikie.


Isa akawaambia, “Amin, nawaambia, wakati wa kufanywa upya vitu vyote, Mwana wa Adamu atakapoketi kwenye kiti chake kitukufu cha enzi, ninyi mlionifuata pia mtaketi katika viti vya enzi kumi na viwili, mkiyahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.


“Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa?


Mvunaji tayari anapokea mshahara wake, naye anakusanya mazao kwa ajili ya uzima wa milele. Ili yeye apandaye na yeye avunaye wafurahi pamoja.


Yahya alikuwa taa iliyowaka na kutoa nuru, nanyi kwa muda mlichagua kuifurahia nuru yake.


Katika kundi la waumini huko Antiokia ya Shamu walikuwako manabii na walimu: yaani Barnaba, Simeoni aitwaye Nigeri, Lukio Mkirene, Manaeni aliyekuwa amelelewa pamoja na Mfalme Herode Agripa, na Sauli.


Kwa neema Mungu aliyonipa, niliweka msingi kama mjenzi stadi na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mmoja inampasa awe mwangalifu jinsi anavyojenga.


Ndiye aliweka wengine kuwa mitume, wengine kuwa manabii, wengine kuwa wainjilisti, wengine kuwa wachungaji na walimu,


Kwa hakika, ingawa mpaka wakati huu ingewapasa kuwa walimu, bado mnahitaji mtu wa kuwafundisha tena hatua za awali za kweli ya Neno la Mungu. Mnahitaji maziwa, wala si chakula kigumu!


Hesabuni uvumilivu wa Bwana Isa kuwa ni wokovu, kama vile ndugu yetu mpenzi Paulo alivyowaandikia kwa hekima ile aliyopewa na Mwenyezi Mungu.


Kuhusu siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume na vile vinara saba vya taa vya dhahabu ni hii: Zile nyota saba ni malaika wa yale makundi saba ya waumini, navyo vile vinara saba ni hayo makundi saba.


“Adui zako wote na waangamie, Ee bwana! Bali wote wakupendao na wawe kama jua lichomozavyo kwa nguvu zake.” Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo