Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Samueli 2:3 - Neno: Maandiko Matakatifu

3 “Msiendelee kusema kwa kiburi hivyo wala msiache vinywa vyenu kunena kwa kiburi, kwa kuwa bwana ndiye Mungu ajuaye, na kwa yeye matendo hupimwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Acheni kujisifu, acheni kusema ufidhuli. Maana ajuaye ni Mwenyezi-Mungu. Yeye huyapima matendo yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Acheni kujisifu, acheni kusema ufidhuli. Maana ajuaye ni Mwenyezi-Mungu. Yeye huyapima matendo yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Acheni kujisifu, acheni kusema ufidhuli. Maana ajuaye ni Mwenyezi-Mungu. Yeye huyapima matendo yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 “Msiendelee kusema kwa kiburi hivyo wala msiache vinywa vyenu kunena kwa kiburi, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu ajuaye, na yeye hupima matendo.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa, Naye huyapima matendo kwa mizani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

3 Acheni kujisifu, acheni kusema ufidhuli. Maana ajuaye ni Mwenyezi-Mungu. Yeye huyapima matendo yote.

Tazama sura Nakili




1 Samueli 2:3
26 Marejeleo ya Msalaba  

basi usikie kutoka mbinguni, katika makao yako. Usamehe na utende, umpe kila mtu kulingana na matendo yake, kwa kuwa unaujua moyo wake (kwa kuwa ni wewe peke yako ujuaye mioyo ya watu wote),


Mungu na anipime katika mizani za uaminifu, naye atajua kwamba sina hatia:


Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi, ufahamu wake hauna kikomo.


Huifunga mioyo yao iliyo migumu, vinywa vyao hunena kwa majivuno.


Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe, kwa maana kwa kiburi na dharau wao husema kwa majivuno dhidi ya wenye haki.


je, Mungu hangaligundua hili, kwa kuwa anazijua siri za moyo?


Msiinue pembe zenu dhidi ya mbingu; msiseme kwa shingo zilizonyooshwa.’ ”


Wanamimina maneno ya kiburi, watenda mabaya wote wamejaa majivuno.


Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na bwana.


Kama mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,” je, yule apimaye mioyo halitambui hili? Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili? Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda?


Kumcha bwana ni kuchukia uovu; ninachukia kiburi na majivuno, tabia mbaya na mazungumzo potovu.


Mapito ya wenye haki yamenyooka. Ewe uliye Mwenye Haki, waisawazisha njia ya mtu mnyofu.


Ni nani uliyemtukana na kumkufuru? Ni nani uliyeinua sauti yako dhidi yake, na kumwinulia macho yako kwa kiburi? Ni dhidi ya yule Aliye Mtakatifu wa Israeli!


“Mimi bwana huchunguza moyo na kuzijaribu nia, ili kumlipa mtu kwa kadiri ya mwenendo wake, kwa kadiri ya matendo yake yanavyostahili.”


Ulijigamba dhidi yangu na kusema maneno dhidi yangu bila kujizuia, nami nikayasikia.


Basi mimi, Nebukadneza, humhimidi, na humtukuza na kumsifu Mfalme wa mbinguni, kwa sababu kila kitu afanyacho ni haki, na njia zake zote ni adili. Nao waendao kwa kiburi anaweza kuwashusha.


“Tekeli: Wewe umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua.


“Mmesema vitu vigumu dhidi yangu,” asema bwana. “Hata hivyo mnauliza, ‘Tumesema nini dhidi yako?’


Kwa maana Neno la Mwenyezi Mungu li hai tena lina nguvu. Lina makali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili, hivyo linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.


“Yeye Mwenye Nguvu, Mungu, bwana! Yeye Mwenye Nguvu, Mungu, bwana! Yeye anajua! Israeli na wajue! Kama huu umekuwa ni uasi au kukosa utii kwa bwana, msituache hai siku hii ya leo.


Nami nitawaua watoto wake. Nayo makundi yote ya waumini yatajua kwamba Mimi ndiye nichunguzaye mioyo na nia, na kwamba nitamlipa kila mmoja wenu kwa kadiri ya matendo yake.


Ndipo Zebuli akamwambia, “Kuko wapi kujivuna kwako sasa, wewe uliyesema, ‘Huyo Abimeleki ni nani hata tumtumikie?’ Hawa si wale watu uliowadharau? Toka nje sasa ukapigane nao!”


Lakini bwana akamwambia Samweli, “Usitazame sura yake wala kimo chake, kwa kuwa nimemkataa. bwana hatazami katika vile vitu mwanadamu avitazamavyo. Mwanadamu hutazama katika sura ya nje, lakini bwana hutazama moyoni.”


Tufuate:

Matangazo


Matangazo