Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




1 Samueli 2:3 - Biblia Habari Njema

3 Acheni kujisifu, acheni kusema ufidhuli. Maana ajuaye ni Mwenyezi-Mungu. Yeye huyapima matendo yote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema - BHND

3 Acheni kujisifu, acheni kusema ufidhuli. Maana ajuaye ni Mwenyezi-Mungu. Yeye huyapima matendo yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Acheni kujisifu, acheni kusema ufidhuli. Maana ajuaye ni Mwenyezi-Mungu. Yeye huyapima matendo yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 “Msiendelee kusema kwa kiburi hivyo wala msiache vinywa vyenu kunena kwa kiburi, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu ajuaye, na yeye hupima matendo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 “Msiendelee kusema kwa kiburi hivyo wala msiache vinywa vyenu kunena kwa kiburi, kwa kuwa bwana ndiye Mungu ajuaye, na kwa yeye matendo hupimwa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo; Majivuno yasitoke vinywani mwenu; Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa, Naye huyapima matendo kwa mizani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

3 Acheni kujisifu, acheni kusema ufidhuli. Maana ajuaye ni Mwenyezi-Mungu. Yeye huyapima matendo yote.

Tazama sura Nakili




1 Samueli 2:3
26 Marejeleo ya Msalaba  

Basi, usikie huko kwako mbinguni, utoe msamaha na kuchukua hatua; pia umtendee kila mtu kadiri anavyostahili (kwani ni wewe tu ujuaye mawazo ya mioyo ya wanadamu wote);


Mungu na anipime katika mizani ya haki, naye ataona kwamba sina hatia.


Bwana wetu ni mkuu, ana nguvu nyingi; maarifa yake hayana kipimo.


Hao hawana huruma yoyote moyoni; wamejaa maneno ya kujigamba.


Izibe midomo ya hao watu waongo, watu walio na kiburi na majivuno, ambao huwadharau watu waadilifu.


ee Mungu, ungalikwisha jua jambo hilo, kwa maana wewe wazijua siri za moyoni.


Msijione kuwa watu wa maana sana, wala kusema maneno ya majivuno.’”


Hata lini waovu watajigamba kwa maneno? Waovu wote watajivuna mpaka lini?


Matendo ya mtu huonekana kwake kuwa sawa, lakini Mwenyezi-Mungu hupima nia ya mtu.


Usiseme baadaye: “Hatukujua!” Maana Mungu apimaye mioyo ya watu huona; yeye atakulipa kulingana na matendo yako!


Kumcha Mwenyezi-Mungu ni kuchukia uovu. Nachukia kiburi, majivuno na maisha mabaya; nachukia na lugha mbaya.


Njia ya watu wanyofu ni rahisi; ewe Mungu mwadilifu, wasawazisha njia yao.


Wewe umemtukana nani? Umemkashifu nani? Umethubutu kumbeza nani kwa majivuno? Ni mimi Mungu, Mtakatifu wa Israeli!


Mimi Mwenyezi-Mungu hupima akili na kuchunguza mpaka ndani ya moyo wa mtu. Na hivyo humtendea kila mmoja, kulingana na mwenendo wake, kadiri ya matendo yake.”


Nimesikia jinsi unavyojigamba na kusema maneno mengi dhidi yangu.


“Na sasa, mimi Nebukadneza ninamsifu na kumtukuza na kumheshimu mfalme wa mbinguni. Maana matendo yake yote ni ya haki, naye huwashusha wenye kiburi.”


TEKELI maana yake, wewe umepimwa katika mizani, nawe ukaonekana huna uzito wowote.


Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Maneno yenu yamekuwa mzigo kwangu. Hata hivyo mnasema, ‘Tumesema nini dhidi yako?’


Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo na roho hukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vya mwili na uboho. Neno hilo huchambua nia na fikira za mioyo ya watu.


“Mungu wa miungu ndiye Mwenyezi-Mungu! Mungu wa miungu ndiye Mwenyezi-Mungu! Yeye anajua kwa nini tumefanya hivyo. Na Waisraeli wote watajua pia! Kama huu ni uasi au ni ukosefu wa imani kwa Mwenyezi-Mungu basi, yeye aache kutuokoa leo.


Tena nitawaua wafuasi wake, ili makanisa yote yatambue kwamba mimi ndiye ninayechunguza mioyo na fikira za watu.


Kisha Zebuli akamwambia, “Majivuno yako yako wapi sasa? Si ni wewe uliyesema, ‘Abimeleki ni nani? Kwa nini tumtumikie?’ Sasa, hao ndio watu uliowadharau; nenda ukapigane nao.”


Lakini Mwenyezi-Mungu alimwambia, “Usiangalie sura yake na urefu wa kimo chake. Mimi nimemkataa kwani siangalii mambo kama wanavyoyaangalia binadamu wenye kufa. Binadamu huangalia uzuri wa nje, lakini mimi naangalia moyoni.”


Tufuate:

Matangazo


Matangazo