Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwasamehe ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utusamehe kosa la watumishi wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye.
Zaburi 81:1 - Swahili Revised Union Version Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha, Mshangilieni Mungu wa Yakobo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwimbieni kwa sauti Mungu, nguvu yetu, mshangilieni Mungu wa Yakobo; Biblia Habari Njema - BHND Mwimbieni kwa sauti Mungu, nguvu yetu, mshangilieni Mungu wa Yakobo; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwimbieni kwa sauti Mungu, nguvu yetu, mshangilieni Mungu wa Yakobo; Neno: Bibilia Takatifu Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu; mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo! Neno: Maandiko Matakatifu Mwimbieni kwa furaha, Mungu aliye nguvu yetu; mpigieni kelele za shangwe Mungu wa Yakobo! BIBLIA KISWAHILI Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha, Mshangilieni Mungu wa Yakobo. |
Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwasamehe ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utusamehe kosa la watumishi wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye.
BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.
Kumbe! Huyu ndiye mtu yule, Asiyemfanya Mungu kuwa kimbilio lake. Aliutumainia wingi wa mali zake, Na kufanya mali kimbilio lake.
Mataifa na washangilie, Naam, waimbe kwa furaha, Maana kwa haki utawahukumu watu, Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
Ee, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;
Maana BWANA asema hivi, Mwimbieni Yakobo kwa furaha, mkampigie kelele mkuu wa mataifa, tangazeni, sifuni, mkaseme, Ee BWANA, uwaokoe watu wako, mabaki ya Israeli.
Mimi ni Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai.