Zaburi 26:2 - Swahili Revised Union Version Ee BWANA, unijaribu na kunipima; Unisafishe akili yangu na moyo wangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Unijaribu, ee Mwenyezi-Mungu, na kunipima; uchunguze moyo wangu na akili zangu. Biblia Habari Njema - BHND Unijaribu, ee Mwenyezi-Mungu, na kunipima; uchunguze moyo wangu na akili zangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Unijaribu, ee Mwenyezi-Mungu, na kunipima; uchunguze moyo wangu na akili zangu. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, unijaribu, unipime, uuchunguze moyo wangu na mawazo yangu; Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, unijaribu, unipime, uuchunguze moyo wangu na mawazo yangu; BIBLIA KISWAHILI Ee BWANA, unijaribu na kunipima; Unisafishe akili yangu na moyo wangu. |
Umenijaribu moyo wangu, umenijia usiku, Umenichunguza usione neno; Nimenuia kinywa changu kisikose,
Ubaya wao wasio haki na ukome, Lakini umthibitishe mwenye haki. Kwa maana mjaribu mioyo na fikira Ndiye Mungu aliye mwenye haki.
Lakini, Ee BWANA wa majeshi, wewe wawajaribu wenye haki, waona fikira na mioyo, nijalie kuona kisasi chako juu yao; kwa maana nimekufunulia wewe neno langu.
Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.