Hata maombolezo hayo yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa, akamtia nyumbani mwake; naye akawa mkewe, akamzalia mtoto wa kiume. Lakini jambo lile alilolitenda Daudi likamchukiza BWANA.
Zaburi 139:3 - Swahili Revised Union Version Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watambua nikienda au nikipumzika; wewe wazijua shughuli zangu zote. Biblia Habari Njema - BHND Watambua nikienda au nikipumzika; wewe wazijua shughuli zangu zote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watambua nikienda au nikipumzika; wewe wazijua shughuli zangu zote. Neno: Bibilia Takatifu Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu; unaelewa njia zangu zote. Neno: Maandiko Matakatifu Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu; unaelewa njia zangu zote. BIBLIA KISWAHILI Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, Umeelewa na njia zangu zote. |
Hata maombolezo hayo yalipokwisha, Daudi akatuma mtu, akamtwaa, akamtia nyumbani mwake; naye akawa mkewe, akamzalia mtoto wa kiume. Lakini jambo lile alilolitenda Daudi likamchukiza BWANA.
Akaweka askari wenye kulinda ngome katika Edomu; katikati ya Edomu yote akaweka ngome, na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye BWANA akampa Daudi ushindi kila kokote alikokwenda.
Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.
Ole wao wanaojitahidi kumficha BWANA mashauri yao, na matendo yao yamo gizani, nao husema, Ni nani atuonaye? Nani atujuaye?
Je, mtu yeyote aweza kujificha mahali pa siri, nisimwone? Asema BWANA. Je! Mbingu na nchi hazikujawa nami? Asema BWANA.
Ambaye pepeto lake li mkononi mwake, naye atausafisha sana uwanda wake; na kuikusanya ngano yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.
Hata wakati wa chakula cha jioni; naye Ibilisi amekwisha kumtia Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti, moyo wa kumsaliti;
Naye alipokwisha kusema hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia akisema, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu atanisaliti.