Zaburi 101:1 - Swahili Revised Union Version Rehema na hukumu nitaziimba, Ee BWANA, nitakuimbia zaburi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utenzi wangu kuhusu uaminifu na haki; ninauimba kwa heshima yako, ee Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Utenzi wangu kuhusu uaminifu na haki; ninauimba kwa heshima yako, ee Mwenyezi-Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utenzi wangu kuhusu uaminifu na haki; ninauimba kwa heshima yako, ee Mwenyezi-Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Nitaimba kuhusu upendo wako na haki yako; kwako wewe, Ee Mwenyezi Mungu, nitaimba sifa. Neno: Maandiko Matakatifu Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako; kwako wewe, Ee bwana, nitaimba sifa. BIBLIA KISWAHILI Rehema na hukumu nitaziimba, Ee BWANA, nitakuimbia zaburi. |
Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu, Uniponye na umwagaji wa damu, Na ulimi wangu utaiimba haki yako.
Fadhili za BWANA nitaziimba milele; Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
Sayuni imesikia na kufurahi, Binti za Yuda walishangilia, Kwa sababu ya hukumu zako, Ee BWANA.
Ee mwanadamu, yeye amekuonesha yaliyo mema; na BWANA anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako!
Tazama, basi, wema na ukali wa Mungu; kwa wale walioanguka, ukali, bali kwako wewe wema wa Mungu, ukikaa katika wema huo; kama sivyo, wewe nawe utakatiliwa mbali.