Yoshua 7:8 - Swahili Revised Union Version Ee Bwana, niseme nini baada ya Israeli kuwapa visogo adui zao? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Bwana, niseme nini hali Waisraeli wamewakimbia adui zao? Biblia Habari Njema - BHND Ee Bwana, niseme nini hali Waisraeli wamewakimbia adui zao? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Bwana, niseme nini hali Waisraeli wamewakimbia adui zao? Neno: Bibilia Takatifu Ee Bwana, niseme nini sasa, ikiwa sasa Israeli ameshafukuzwa na adui zake? Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, niseme nini sasa, ikiwa sasa Israeli ameshafukuzwa na adui zake? BIBLIA KISWAHILI Ee Bwana, niseme nini baada ya Israeli kuwapa visogo adui zao? |
Mimi nitasimama katika zamu yangu, nitajiweka juu ya mnara, nitaangalia ili nione atakaloniambia, na jinsi nitakavyojibu kuhusu kulalamika kwangu.
Yoshua akasema, Ee Bwana MUNGU, kwa nini umewavusha watu hawa mto wa Yordani, ili kututia katika mikono ya Waamori, na kutuangamiza? Laiti tu, tungaliridhika kukaa ng'ambo ya Yordani
Maana Wakanaani na wenyeji wote wa nchi hii watasikia habari hii, nao watatuzingira, na kulifuta jina letu katika nchi. Nawe utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?
Hata watu walipofika kambini, wazee wa Israeli wakasema, Mbona BWANA ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende tukalilete sanduku la Agano la BWANA kutoka Shilo hadi huku, lije kati yetu, na kutuokoa katika mikono ya adui zetu.