Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wakiumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, nduguze Dina, wakatwaa kila mtu upanga wake, wakaujia mji kwa ujasiri, wakawaua wanaume wote.
Yoshua 5:8 - Swahili Revised Union Version Ilikuwa walipokwisha kutahiriwa taifa zima, wakakaa kila mtu mahali pake kambini, hadi walipopoa. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanaume wote walipokwisha tahiriwa walikaa katika sehemu zao humo kambini mpaka walipopona. Biblia Habari Njema - BHND Wanaume wote walipokwisha tahiriwa walikaa katika sehemu zao humo kambini mpaka walipopona. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanaume wote walipokwisha tahiriwa walikaa katika sehemu zao humo kambini mpaka walipopona. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya taifa lote kutahiriwa, waliendelea kukaa kambini hadi walipopona. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya taifa lote kutahiriwa, waliendelea kukaa kambini mpaka walipokuwa wamepona. BIBLIA KISWAHILI Ilikuwa walipokwisha kutahiriwa taifa zima, wakakaa kila mtu mahali pake kambini, hadi walipopona. |
Ikawa siku ya tatu, walipokuwa wakiumwa sana, wana wawili wa Yakobo, Simeoni na Lawi, nduguze Dina, wakatwaa kila mtu upanga wake, wakaujia mji kwa ujasiri, wakawaua wanaume wote.
Na watoto wao, aliowainua badala yao ndio hao aliowatahiri Yoshua; kwa kuwa wao walikuwa hawajatahiriwa, kwa maana hawakuwatahiri njiani.
BWANA akamwambia Yoshua, Siku hii ya leo nimeivingirisha hiyo aibu ya Misri iondoke juu yenu. Kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Gilgali, hata hivi leo.