Ee BWANA, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na ushindi, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.
Yoshua 3:13 - Swahili Revised Union Version Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukuao sanduku la BWANA, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yataacha kutiririka, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama kichuguu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wakati nyayo za makuhani wanaobeba sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Bwana wa dunia yote, zitakapoingia katika maji ya mto Yordani, maji ya mto huo yataacha kutiririka. Na yale yatakayokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yatajikusanya pamoja kama rundo.” Biblia Habari Njema - BHND Wakati nyayo za makuhani wanaobeba sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Bwana wa dunia yote, zitakapoingia katika maji ya mto Yordani, maji ya mto huo yataacha kutiririka. Na yale yatakayokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yatajikusanya pamoja kama rundo.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wakati nyayo za makuhani wanaobeba sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Bwana wa dunia yote, zitakapoingia katika maji ya mto Yordani, maji ya mto huo yataacha kutiririka. Na yale yatakayokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yatajikusanya pamoja kama rundo.” Neno: Bibilia Takatifu Mara tu nyayo za makuhani walichukualo Sanduku la Mwenyezi Mungu, Bwana wa dunia yote, zitakapokanyaga ndani ya Mto Yordani, maji hayo yanayotiririka kutoka juu yatatindika na kusimama kama chuguu.” Neno: Maandiko Matakatifu Mara tu nyayo za makuhani walichukualo Sanduku la bwana, Bwana wa dunia yote, zitakapokanyaga ndani ya Mto Yordani, maji hayo yatiririkayo kutoka juu yatatindika na kusimama kama chuguu.” BIBLIA KISWAHILI Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukuao sanduku la BWANA, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yataacha kutiririka, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama kichuguu. |
Ee BWANA, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na ushindi, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.
Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa kilima, Vilindi vikagandamana katikati ya bahari.
Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.
Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili watiwa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.
Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani yaliondoka mbele ya sanduku la Agano la BWANA; hapo lilipovuka Yordani, hayo maji ya Yordani yalisimama; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa Israeli milele.