Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 3:13 - Swahili Revised Union Version

13 Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukuao sanduku la BWANA, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yataacha kutiririka, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama kichuguu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Wakati nyayo za makuhani wanaobeba sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Bwana wa dunia yote, zitakapoingia katika maji ya mto Yordani, maji ya mto huo yataacha kutiririka. Na yale yatakayokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yatajikusanya pamoja kama rundo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Wakati nyayo za makuhani wanaobeba sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu, Bwana wa dunia yote, zitakapoingia katika maji ya mto Yordani, maji ya mto huo yataacha kutiririka. Na yale yatakayokuwa yanatiririka kutoka upande wa juu yatajikusanya pamoja kama rundo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Mara tu nyayo za makuhani walichukualo Sanduku la Mwenyezi Mungu, Bwana wa dunia yote, zitakapokanyaga ndani ya Mto Yordani, maji hayo yanayotiririka kutoka juu yatatindika na kusimama kama chuguu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Mara tu nyayo za makuhani walichukualo Sanduku la bwana, Bwana wa dunia yote, zitakapokanyaga ndani ya Mto Yordani, maji hayo yatiririkayo kutoka juu yatatindika na kusimama kama chuguu.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

13 Itakuwa, wakati nyayo za makuhani walichukuao sanduku la BWANA, Bwana wa dunia yote, zitakaposimama katika maji ya Yordani, hayo maji ya Yordani yataacha kutiririka, maji yale yashukayo kutoka juu; nayo yatasimama kama kichuguu.

Tazama sura Nakili

Yoshua 3:13
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ee BWANA, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na ushindi, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee BWANA, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote.

Hukusanya maji ya bahari chungu chungu, Huviweka vilindi katika ghala.

Wewe ulitokeza chemchemi na kijito; Wewe ulikausha mito yenye maji sikuzote.

Aliipasua bahari akawavusha; Aliyafanya maji yasimame kama ukuta.

Kwa upepo wa mianzi ya pua yako maji yalipandishwa, Mawimbi yakasimama juu wima mfano wa kilima, Vilindi vikagandamana katikati ya bahari.

Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.

Ukaikanyaga bahari kwa farasi wako, Chungu ya maji yenye nguvu.

Ndipo akasema, Hivi ni hao wana wawili watiwa mafuta, wasimamao karibu na Bwana wa dunia yote.

Tazama, sanduku la Agano la Bwana wa dunia yote linavuka mbele yenu na kuingia Yordani.

Ndipo mtakapowaambia, Ni kwa sababu maji ya Yordani yaliondoka mbele ya sanduku la Agano la BWANA; hapo lilipovuka Yordani, hayo maji ya Yordani yalisimama; na mawe haya yatakuwa ni ukumbusho kwa wana wa Israeli milele.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo