Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yoshua 23:3 - Swahili Revised Union Version

nanyi mmeona mambo yote ambayo BWANA, Mungu wenu, amewatenda mataifa haya yote kwa ajili yenu; kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye aliyewapigania ninyi.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Nyinyi mmeona mambo yote Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliyoyatendea mataifa haya yote kwa ajili yenu. Mwenyezi-Mungu Mungu wenu ndiye aliyewapigania.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Nyinyi mmeona mambo yote Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliyoyatendea mataifa haya yote kwa ajili yenu. Mwenyezi-Mungu Mungu wenu ndiye aliyewapigania.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Nyinyi mmeona mambo yote Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliyoyatendea mataifa haya yote kwa ajili yenu. Mwenyezi-Mungu Mungu wenu ndiye aliyewapigania.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ninyi wenyewe mmeona kila kitu Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alichowatendea mataifa haya yote kwa ajili yenu. Ilikuwa ni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, aliyewapigania.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ninyi wenyewe mmeona kila kitu bwana Mwenyezi Mungu wenu, alichowatendea mataifa haya yote kwa ajili yenu. Ilikuwa ni bwana Mwenyezi Mungu wenu aliyewapigania.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

nanyi mmeona mambo yote ambayo BWANA, Mungu wenu, amewatenda mataifa haya yote kwa ajili yenu; kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye aliyewapigania ninyi.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yoshua 23:3
13 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.


Mmeona jinsi nilivyowatendea Wamisri, na jinsi nilivyowachukua ninyi juu ya mbawa za tai, nikawaleta ninyi kwangu mimi.


Kwa maana nilipokuwa nimekwisha kuwaingiza katika nchi ile, ambayo niliuinua mkono wangu kuwapa, wakati huo walipoona kila mlima mrefu, na kila mti wenye majani mengi, walitoa matoleo yao huko, na huko walitoa chukizo la sadaka zao, na huko walifukiza manukato ya kupendeza, na huko walimimina sadaka zao za kunywewa.


Na macho yenu ninyi yataona, nanyi mtasema, BWANA ndiye mkuu hata katika nje ya mipaka ya Israeli.


BWANA, Mungu wenu, anayetangulia mbele yenu, ndiye atakayewapigania, kwa mfano wa yote aliyowafanyia huko Misri mbele ya macho yenu;


kwa maana BWANA, Mungu wenu, ndiye awaandamaye kwenda kuwapigania juu ya adui zenu, ili kuwaokoa ninyi.


Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako;


Nawe kama ukisema moyoni mwako, Mataifa haya ni mengi kuliko mimi; nitawatoaje katika milki yao?


Na wafalme wao atakutilia mkononi mwako, nawe utalipoteza jina lao litoke chini ya mbingu; hapana mtu atakayeweza kusimama mbele yako, hata utakapokwisha kuwaangamiza.


Haikuwapo siku nyingine mfano wa siku hiyo katika siku zilizotangulia mbele yake wala katika hizo zilizofuata baada yake, hata ikawa yeye BWANA kuisikia sauti ya binadamu; kwa kuwa BWANA alipiga vita kwa ajili ya Israeli.


Na wafalme hao wote na nchi zao Yoshua akatwaa kwa wakati mmoja, kwa sababu yeye BWANA, Mungu wa Israeli, alipigana kwa ajili ya Israeli,


Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana BWANA, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia.