Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Malaki 1:5 - Swahili Revised Union Version

5 Na macho yenu ninyi yataona, nanyi mtasema, BWANA ndiye mkuu hata katika nje ya mipaka ya Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Nanyi mtakapoyaona hayo kwa macho yenu, mtatambua na kusema: ‘Ukuu wa Mwenyezi-Mungu wafika hata nje ya mipaka ya nchi ya Israeli.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Nanyi mtakapoyaona hayo kwa macho yenu, mtatambua na kusema: ‘Ukuu wa Mwenyezi-Mungu wafika hata nje ya mipaka ya nchi ya Israeli.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Nanyi mtakapoyaona hayo kwa macho yenu, mtatambua na kusema: ‘Ukuu wa Mwenyezi-Mungu wafika hata nje ya mipaka ya nchi ya Israeli.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Mtayaona kwa macho yenu wenyewe na kusema, ‘Mwenyezi Mungu ni mkuu, hata nje ya mipaka ya Israeli!’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Mtayaona kwa macho yenu wenyewe na kusema, ‘bwana ni mkuu, hata nje ya mipaka ya Israeli!’

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Na macho yenu ninyi yataona, nanyi mtasema, BWANA ndiye mkuu hata katika nje ya mipaka ya Israeli.

Tazama sura Nakili




Malaki 1:5
14 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa hiyo hasira ya BWANA imekuwa juu ya Yuda na Yerusalemu, naye amewatoa kuwa matetemeko, wawe ushangao, na mazomeo, kama muonavyo kwa macho yenu.


nawe utapanda juu uwajie watu wangu, Israeli, kama wingu likiifunika nchi; itakuwa katika siku za mwisho, nitakuleta upigane na nchi yangu, ili mataifa wanijue, nitakapotakaswa kupitia kwako, Ewe Gogu, mbele ya macho yao.


Nami nitajitukuza, na kujitakasa, na kujidhihirisha, mbele ya macho ya mataifa mengi; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.


Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka, nao watafanya mioto kwa silaha za vita na kuziteketeza, ngao, na vigao, na pinde, na mishale, na mafumo, na mikuki, nao watazitumia kama kuni kwa muda wa miaka saba;


Naye atasimama, na kulisha kundi lake kwa nguvu za BWANA, kwa enzi ya jina la BWANA, Mungu wake; nao watakaa; maana sasa atakuwa mkuu hadi miisho ya dunia.


lakini macho yenu yameiona kazi kubwa ya BWANA aliyoifanya, yote.


Macho yenu yameona aliyoyatenda BWANA kwa sababu ya Baal-peori; maana wote waliomfuata Baal-peori, BWANA, Mungu wako, amewaangamiza kutoka kati yako.


Nao walipomlilia BWANA, akaweka giza kati yenu na Wamisri, akaileta bahari juu yao, akawafunikiza; nayo macho yenu yaliyaona mambo niliyoyatenda huko Misri; kisha mkakaa jangwani siku nyingi.


Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, BWANA atakalolitenda mbele ya macho yenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo