naye akawaambia, Ninyi mmeyafuata hayo yote mliyoamriwa na Musa, mtumishi wa BWANA, nanyi mmeisikia sauti yangu katika yote niliyowaamuru mimi;
Yoshua 22:3 - Swahili Revised Union Version hamkuwaacha hao ndugu zenu siku hizi nyingi hata hivi leo, lakini mmeyashika maagizo ya amri ya BWANA, Mungu wenu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wala hamkuwaacha ndugu zenu muda huo wote mrefu mpaka leo, bali mmefuata kwa makini amri ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Biblia Habari Njema - BHND Wala hamkuwaacha ndugu zenu muda huo wote mrefu mpaka leo, bali mmefuata kwa makini amri ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wala hamkuwaacha ndugu zenu muda huo wote mrefu mpaka leo, bali mmefuata kwa makini amri ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa muda mrefu sasa, hadi siku hii ya leo, hamkuwaacha ndugu zenu, bali ninyi mmetimiza ile kazi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, aliyowapa. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa muda mrefu sasa, hadi siku hii ya leo, hamkuwaacha ndugu zenu, bali ninyi mmetimiza ile kazi bwana Mwenyezi Mungu wenu aliyowapa. BIBLIA KISWAHILI hamkuwaacha hao ndugu zenu siku hizi nyingi hata hivi leo, lakini mmeyashika maagizo ya amri ya BWANA, Mungu wenu. |
naye akawaambia, Ninyi mmeyafuata hayo yote mliyoamriwa na Musa, mtumishi wa BWANA, nanyi mmeisikia sauti yangu katika yote niliyowaamuru mimi;
Na sasa yeye BWANA, Mungu wenu, amewapa ndugu zenu kustarehe, kama alivyowaambia; basi sasa rudini ninyi mwende mahemani kwenu, hata nchi ya milki yenu, ambayo huyo Musa, mtumishi wa BWANA, aliwapa ng'ambo ya pili ya Yordani.