Yoshua 21:5 - Swahili Revised Union Version Kisha Wakohathi wengine waliosalia walipata kwa kura miji kumi katika jamaa za kabila la Efraimu, na katika kabila la Dani, na katika hiyo nusu ya kabila la Manase. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa ukoo wa Kohathi waliosalia walipewa miji kumi iliyoko katika maeneo ya makabila ya Efraimu, Dani na katika eneo la nusu ya kabila la Manase. Biblia Habari Njema - BHND Watu wa ukoo wa Kohathi waliosalia walipewa miji kumi iliyoko katika maeneo ya makabila ya Efraimu, Dani na katika eneo la nusu ya kabila la Manase. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa ukoo wa Kohathi waliosalia walipewa miji kumi iliyoko katika maeneo ya makabila ya Efraimu, Dani na katika eneo la nusu ya kabila la Manase. Neno: Bibilia Takatifu Wazao wengine waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za makabila ya Efraimu, Dani na nusu ya Manase. Neno: Maandiko Matakatifu Wazao wengine waliobaki wa Wakohathi walipewa miji kumi kutoka koo za makabila ya Efraimu, Dani na nusu ya Manase. BIBLIA KISWAHILI Kisha Wakohathi wengine waliosalia walipata kwa kura miji kumi katika jamaa za kabila la Efraimu, na katika kabila la Dani, na katika hiyo nusu ya kabila la Manase. |
Nao waliobaki wa wana wa Kohathi walipewa kwa kura miji kumi, katika jamaa ya kabila hilo, yaani, nusu kabila, nusu ya Manase.
Na katika Kohathi ni jamaa ya Waamrami, na jamaa ya Waishari, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya hao Wauzieli; hizo ni jamaa za Wakohathi.
Kura ikatokea kwa ajili ya jamaa za Wakohathi; na wana wa Haruni kuhani, waliokuwa katika Walawi, walipata miji kumi na mitatu kwa kura katika kabila la Yuda, na katika kabila la Simeoni, na katika kabila la Benyamini.
Tena wana wa Gershoni walipata kwa kura miji kumi na mitatu katika jamaa za kabila la Isakari, na katika kabila la Asheri, na katika kabila la Naftali, na katika hiyo nusu ya kabila la Manase huko Bashani.