Basi haya ndiyo makao yao, kwa kufuata mipaka ya kambi zao; wana wa Haruni, katika jamaa za Wakohathi; kwani walikuwa na kura ya kwanza;
Yoshua 21:10 - Swahili Revised Union Version nayo ilikuwa kwa ajili ya wana wa Haruni, wa jamaa ya Wakohathi, waliokuwa wa wana wa Lawi; kwa kuwa kura ya kwanza ilikuwa ni yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema wazawa wa kuhani Aroni, waliokuwa jamaa za ukoo wa Kohathi ambaye alikuwa wa kabila la Lawi. Sehemu yao walipata kwanza kwani kura yao ilitokea kwanza. Biblia Habari Njema - BHND wazawa wa kuhani Aroni, waliokuwa jamaa za ukoo wa Kohathi ambaye alikuwa wa kabila la Lawi. Sehemu yao walipata kwanza kwani kura yao ilitokea kwanza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza wazawa wa kuhani Aroni, waliokuwa jamaa za ukoo wa Kohathi ambaye alikuwa wa kabila la Lawi. Sehemu yao walipata kwanza kwani kura yao ilitokea kwanza. Neno: Bibilia Takatifu (miji hii walipewa wazao wa Haruni ambao walitokana na koo za Wakohathi wa Walawi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia): Neno: Maandiko Matakatifu (miji hii walipewa wazao wa Haruni ambao walitokana na koo za Wakohathi wa Walawi, kwa sababu kura ya kwanza iliwaangukia): BIBLIA KISWAHILI nayo ilikuwa kwa ajili ya wana wa Haruni, wa jamaa ya Wakohathi, waliokuwa wa wana wa Lawi; kwa kuwa kura ya kwanza ilikuwa ni yao. |
Basi haya ndiyo makao yao, kwa kufuata mipaka ya kambi zao; wana wa Haruni, katika jamaa za Wakohathi; kwani walikuwa na kura ya kwanza;
Na wana wa Kohathi; ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli; na miaka ya maisha ya huyo Kohathi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na mitatu.
Na katika Kohathi ni jamaa ya Waamrami, na jamaa ya Waishari, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya hao Wauzieli; hizo ni jamaa za Wakohathi.
Katika wana wa Lawi uitenge hesabu ya wana wa Kohathi, kwa jamaa zao, na nyumba za baba zao,
Nao wakawapa Kiriath-arba, ndio Hebroni, (huyo Arba alikuwa baba yake Anaki), katika nchi ya vilima ya Yuda, pamoja na mbuga zake za malisho yaliyouzunguka pande zote.
Kura ikatokea kwa ajili ya jamaa za Wakohathi; na wana wa Haruni kuhani, waliokuwa katika Walawi, walipata miji kumi na mitatu kwa kura katika kabila la Yuda, na katika kabila la Simeoni, na katika kabila la Benyamini.
Kisha wakawapa katika kabila la wana wa Yuda, na katika kabila la wana wa Simeoni, miji hii iliyotajwa hapa kwa majina;