Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Yoshua 2:10 - Swahili Revised Union Version

Maana tumesikia jinsi BWANA alivyoyakausha maji ya Bahari ya Shamu mbele yenu, hapo mlipotoka Misri, tena mambo hayo mliyowatendea wafalme wawili wa Waamori waliokuwa huko ng'ambo ya Yordani, yaani, Sihoni na Ogu, mliowaangamiza kabisa.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Maana tumesikia jinsi Mwenyezi-Mungu alivyoyakausha maji ya bahari ya Shamu mbele yenu mlipotoka nchi ya Misri, na jinsi mlivyowatendea wafalme wawili wa Waamori waliokuwa ngambo ya mto Yordani, yaani Sihoni na Ogu, ambao mliwaangamiza kabisa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Maana tumesikia jinsi Mwenyezi-Mungu alivyoyakausha maji ya bahari ya Shamu mbele yenu mlipotoka nchi ya Misri, na jinsi mlivyowatendea wafalme wawili wa Waamori waliokuwa ngambo ya mto Yordani, yaani Sihoni na Ogu, ambao mliwaangamiza kabisa.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Maana tumesikia jinsi Mwenyezi-Mungu alivyoyakausha maji ya bahari ya Shamu mbele yenu mlipotoka nchi ya Misri, na jinsi mlivyowatendea wafalme wawili wa Waamori waliokuwa ng'ambo ya mto Yordani, yaani Sihoni na Ogu, ambao mliwaangamiza kabisa.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Tumesikia jinsi Mwenyezi Mungu alivyokausha maji ya Bahari ya Shamu kwa ajili yenu mlipotoka Misri, pia lile mlilowatendea Sihoni na Ogu, wafalme wawili wa Waamori mashariki mwa Yordani, ambao mliwaangamiza kabisa.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Tumesikia jinsi bwana alivyokausha maji ya Bahari ya Shamu kwa ajili yenu mlipotoka Misri, pia lile mlilowatendea Sihoni na Ogu, wafalme wawili wa Waamori mashariki mwa Yordani, ambao mliwaangamiza kabisa.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Maana tumesikia jinsi BWANA alivyoyakausha maji ya Bahari ya Shamu mbele yenu, hapo mlipotoka Misri, tena mambo hayo mliyowatendea wafalme wawili wa Waamori waliokuwa huko ng'ambo ya Yordani, yaani, Sihoni na Ogu, mliowaangamiza kabisa.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Yoshua 2:10
13 Marejeleo ya Msalaba  

Wewe ulitokeza chemchemi na kijito; Wewe ulikausha mito yenye maji sikuzote.


Kisha Musa akatuma wajumbe kutoka Kadeshi wamwendee mfalme wa Edomu, na kusema, Ndugu yako Israeli asema, Wewe wazijua taabu zote zilizotupata;


Mungu amewaleta kutoka Misri, Naye ana nguvu kama nguvu za nyati.


Mungu amemleta kutoka Misri, Ana nguvu mfano wa nguvu za nyati; Atawameza mataifa walio adui zake, Ataivunja mifupa yao vipande vipande. Atawachoma kwa mishale yake.


Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni hakutuacha kupitia kwake; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, alifanya roho yake kuwa ngumu, akamtia ukaidi moyoni mwake, apate kumtia mkononi mwako kama alivyo hivi leo.


Nikatuma nyigu mbele yenu, waliowafukuza mbele yenu hao wafalme wawili wa Waamori, si kwa upanga wako, wala kwa upinde wako.


watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa BWANA, ya kuwa ni mkono wenye uweza, na ili nanyi mpate kumcha BWANA, Mungu wenu, milele.


Ikawa, wafalme wa Waamori, waliokaa ng'ambo ya Yordani pande za magharibi, na wafalme wote wa Wakanaani, waliokuwa karibu na bahari, waliposikia jinsi BWANA alivyoyakausha maji ya Yordani mbele ya wana wa Israeli, hadi tulipokwisha kuvuka, basi mioyo yao iliyeyuka, wala haikuwamo roho ya nguvu ndani yao tena; kwa ajili ya wana wa Israeli.


na habari ya hayo yote aliyowatenda wale wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa huko ng'ambo ya pili ya Yordani, maana huyo Sihoni, mfalme wa Heshboni, na Ogu, mfalme wa Bashani, aliyekuwa huko Ashtarothi.